Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, November 10, 2015

Mbwezeren: Dk. Shein Rais halali, anaepinga aende mahakamani.

Mwenyekiti wa Zec, Jecha Salim Jecha.
Wanasiasa na wanasheria Zanzibar wameshauriwa kufungua kesi ya Katiba mahakamani kama kweli serikali ya awamu ya saba imefikia kikomo cha kuendelea kubakia madarakani badala ya kuendelea kulalamika katika majukwaa ya kisiasa visiwani humo.
Wito huo ulitolewa na Mwanasheria Mkuu wa zamani za Zanzibar, Hamid Mbwezeren, siku moja tangu mawaziri sita na manaibu waziri watatu wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kutoka Chama cha Wananchi (Cuf) kuamua kujivua nyadhifa zao kwa madai serikali ya awamu ya saba inayoongozwa na Rais Dk. Ali Mohamed Shein (CCM), imemaliza muda wake tangu Novemba 2, mwaka huu.
Alisema jukumu la kutafsiri Katiba na sheria ni kazi ya mahakama, hivyo wanaona Dk. Shein hastahili kuendelea kuwa Rais wafungue kesi kwani ndiyo njia pekee na sahihi ya kupata ukweli juu ya suala hilo.
“Kwa bahati mbaya vifungu vya Katiba cha 28(1) na 28 (2)(a) vimekuwa vikitafasiriwa kwa mtazamo na utashi wa kisiasa na viongozi wa kisiasa pamoja na baadhi ya wanasheria kwa maslahi yao ya kisiasa.”
“Kila chama kina wanasheria lakini wameshindwa kutumia fursa ya mahakama kutafuta ufumbuzi kwa njia halali za kikatiba na sheria,” alisema.
Mwanasheria mkuu huyo wa zamani wa Zanzibar alisisitiza kuwa, kimsingi serikali ya Dk. Shein bado ipo kihalali kwa mujibu wa kifungu cha 28 (1) hadi hapo uchaguzi mwingine utakapoifanyika na kupatikana Rais mpya wa awamu ya nane Zanzibar.
Hata hivyo, Mbwezeren alisema kwamba Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec) inapaswa kukaa pamoja na wadau wake na kuwapatia muongozo wa kinachoendelea tangu ilipofuta matokeo ya uchaguzi huo ili kuondoa sintofahamu.
Alisema wananchi wa Zanzibar pia wanahitaji kujua tarehe ya uchaguzi wa marudio, hatua ambayo itasadia kuondoa uvumi mbalimbali unaoendelea kujitokeza tangu kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi huo.
Umeibuka mjadala mkubwa kuhusu ukomo wa serikali ya awamu ya saba tangu Mwenyekiti wa Zec, Jecha Salim Jecha, alipotangaza kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu Oktoba 28, mwaka huu, kwa madai ya kufanyika udanganyifu, ikiwamo idadi ya kura kuongezeka kuliko idadi ya watu waliosajiliwa katika vituo vya wapiga kura, pamoja na baadhi ya kura kufutwa na kuandikwa sehemu nyingine.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment