Tukio hilo lilitokea juzi, saa 4:00 usiku, baada ya watu wasiojulikana wakiwa na silaha za moto kufika katika eneo hilo na kuanza kuvunja mabanda na mabechi ya kukalia.
Wakizungumza na Nipashe mjini Zanzibar jana, baadhi ya wakazi wa eneo hilo walisema watu wasiojulikana wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 20 waliovunja baraza hiyo kwa kutumia vyuma vya kuvunjia vitu vizito ikiwamo mitalimbo.
“Walipofika walianza kuvunja kibanda kinachotumika kutoa huduma za simu pamoja na fedha na kukipakia katika gari. Tuliwaona wakipakia seti ya televisheni katika gari waliyoitoa katika baraza hiyo,” alisema mmoja wa mashuhuda, Ali Hussen, mkazi wa eneo hilo.
Alisema walipomaliza kuvunja na kupakia vitu hivyo katika gari, wakisindikizwa watu wenye silaha waliovaa kiraia na walipokuwa wakiondoka katika eneo hilo walikatakata mapambo ya vitambaa vya Cuf.
Naibu Katibu wa baraza hiyo, Omar Mussa Makame, alithibitisha kuvamiwa huko na kung’olewa mapambo na picha zote za Maalim Seif.
Alisema wameripoti tukio hilo Kituo cha Polisi Mwembe Madema, Zanzibar na kwamba ni la pili kutokea katika baraza hiyo tangu kuanzishwa kwake.
Juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mkadam Khamisi, hazikufanikiwa baada ya wasaidizi wake kueleza yupo katika shughuli za kazi nje ya ofisi.
CHANZO: THE GUARDIAN
No comments :
Post a Comment