Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo na Nipashe kupata nakala yake, Mfilisi Mohamed, ameeleza kuwa habari hizo ni za uongo na hazina ushahidi wowote na kwamba zimekuwa zikisambazwa na watu wenye chuki na wivu wa kibiashara wakiwa na lengo la kuichonganisha kampuni hiyo na Watanzania ili waichukie serikali yao.
Imeeleza kuwa kampuni hiyo imekuwa ikifanya kazi kwa kuzingatia sheria zote za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tangu ilipoanzishwa. Soma tangazo la habari hii ukurasa wa tano.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment