Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, amewapa mwezi mmoja watumishi wa umma wawe wamejaza fomu za tamko la mali na madeni yao na ambaye hatafanya hivyo atachukuliwa hatua za kisheria na kinidhamu.
Mbali na agizo hilo, watumishi wa umma wamekuwa wakibanwa na hatua za Rais John Magufuli za ubanaji matumizi ya serikali ambapo masuala kama ya safari zisizo za lazima na vikao vya kuhalalisha posho vimefutwa.
Balozi Sefue alitoa rai hiyo jijini Dar es Salaam, wakati akifungua mdahalo unaohusu Umuhimu wa Maadili kwa Maendeleo ya Taifa, katika kuadhimisha siku ya maadili nchini, uliohusisha viongozi wa taasisi za serikali, viongozi wa dini, vyama vya siasa, asasi za kiraia na wanafunzi wa vyuo vikuu.
Alisema Baraza la Maadili litawaita viongozi na watumishi wa umma watakaoshindwa kutekeleza wajibu wao wa kujaza fomu hizo ili wajieleze na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria ikiwamo kuwabaini wale wote walioainisha taarifa za uongo.
“Tukumbuke kuwa ujazaji wa tamko hilo ni wajibu wa kisheria na siyo jambo la hiyari.
Nimeambiwa kuwa wapo wanaojaza fomu kwa kulipua ili mradi kutimiza wajibu, wengine wanaficha baadhi ya mali na kuamini kuwa hakuna atakayefuatilia, wanajidanganya,” alisema Balozi Sefue.
“Nawasihi wasijidanganye, siku isiyo na jina tutafuatilia. Na kwa sababu tuna sheria ya kuwalinda watoa taarifa na mashahidi, naamini wananchi wengi watatupa taarifa pale wanapoona dhahiri kuwa utajiri alionao mtumishi wa umma au kiongozi wa kisiasa haulingani na kipato chake halali,” alisema Balozi Sefue.
Balozi Sefue alisema serikali haitapatia zabuni kampuni ambazo hayajasaini ahadi ya Uadilifu, iliyoanzishwa kwa lengo la kuhusisha ulipaji kodi, vita dhidi ya rushwa, utii wa sheria na kanuni za kuendesha biashara husika.
Balozi Sefue alisema ili kampuni zilizojiwekea ahadi ya maadili yasiathirike kwenye ushindani wa kibiashara, ni muhimu ahadi hiyo itolewe pia na washindani wao.
Aidha, Balozi Sefue aliwataka Watanzania kushirikiana na Rais John Magufuli kuzingatia maadili kama ambavyo walishirikiana naye kufanya usafi na kuliletea Taifa heshima.
“Jana (juzi) tumeionyesha dunia tunachoweza kufanya kwa kusafisha mazingira, tuwaonyeshe tena tunachoweza kufanya kuondoa aibu ya nchi yetu kuwa ya rushwa, dawa za kelevya, ujangili na ukwepaji kodi,” alisema Balozi Sefue.
Kwa upande wake, mshiriki wa mdahalo huo, Mwenyekiti wa Maofisa Watendaji Wakuu wa kampuni Ally Mufuruki aliishukuru serikali kwa kuweka msimamo kuhusu kampuni ambazo hazijaweka ahadi ya uadilifu, kunyimwa zabuni.
Pia alisema suala la ukiukwaji maadili limekuwa janga la Taifa kuanzia ngazi ya familia kutokana na wazazi kuwalinda vijana wao wanaojipatia mali kwa njia zisizo halali pamoja vijana kuamini ofisi za umma kuwa ni sehemu za kujilimbikizia mali.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
No comments :
Post a Comment