Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, December 13, 2015

Muhongo aahidi kushusha bei umeme

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amewahakikishia Watanzania kwamba umeme utashuka bei na hakutakuwa na mgawo.

Akizungumza na waandishi wa habari Ikulu jana mara baada ya kuapishwa, Muhongo alisema tutahakikisha kunakuwa na vyanzo vingi vya umeme ili kuwa na nishati ya uhakika.

Profesa Muhongo alisema wizara yake itajitahidi kuachana na kutegemea vyanzo vya umeme na  watajikita kwenye kufua umeme wa upepo, nishati ya gesi na makaa ya mawe, vyanzo ambavyo vitasaidia kuongeza umeme.

Alisema katika kipindi cha miaka 10 watahakikisha  wanazalisha umeme wa kutosha kuanzia megawati 10,000 hadi 15,000 hadi ifikapo mwaka 2025.

Profesa Muhongo alisema Wakala wa Umeme Vijijini (Rea) wataendelea kuwaunganishia wananchi umeme na atakuwa anatoa taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya wizara yake katika kipindi cha miaka miwili, mitano na kuendelea ili wananchi waelewe.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments :

Post a Comment