Rais John Magufuli jana aliwaapisha mawaziri wake Ikulu jijini Dar es Salaam, huku kukiwa hakuna shamra shamra wala mbwembwe zilizokuwa zimezoeleka wakati wa awamu nne zilizopita.
Ukimya ulitawala zoezi zima la kuapishwa kwa mawaziri hao tofauti na miaka iliyopita na wala hakukuwa na harakati za mawaziri hao kupewa mashada ya maua na kuvalishwa mataji.
Idadi ya wageni waalikwa ilikuwa ndogo sana kulinganisha na utitiri wa watu uliozoeleka Ikulu wakati wa kuapishwa kwa mawaziri, na hasa wakati wa serikali ya awamu ya nne ya Jakaya Kikwete.
Wakati huo ilikuwa kawaida kwa waziri anayeapishwa kuongozana na mke au mume, watoto, ndugu, jamaa, majirani na hata marafiki kwenda Ikulu kwa ajili ya kumpongeza kwa mbwembwe za mashada na maua.
Lakini katika tukio la jana, mbwembwe hizo hazikuwapo.
Tangu kuapishwa kwake Novemba 5, Rais Magufuli amejipambanua kama kiongozi anayechukia matumizi yasiyo ya lazima baada ya kuamuru fedha za hafla ya uzinduzi wa Bunge la 11 zikanunue mahitaji muhimu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Aidha, aliamua Sh. Bilioni 4 zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe za Uhuru zijengewe barabara ya km 4 ya Morocco-Mwenge jijini Dar es Salaam kwa kiwango cha lami.
Aidha, aliamuru wakati akitangaza Baraza lake la Mawaziri katikati ya wiki kwamba fedha za semina elekezi kwa watumishi hao zilizojitokeza awamu ya Kikwete, Sh. bilioni 2, zitapangiwa matumizi na viongozi hao wajifunze juu kwa juu.
Mawaziri hao walianza kuingia Ikulu majira ya saa 3:00 asubuhi na uchunguzi wa Nipashe, ambalo lilifika mapema maeneo hayo, ulionyesha kuwa hawakuwa na msururu wa watu wakati wakiingia.
Mawaziri wengi walioshuhudiwa wakiingia katika lango la Ikulu walionekana kuwa na mgeni mmoja mmoja hali inayoashiria kuwa huenda Ikulu ilidhibiti utitiri wa watu.
Mpaka kufikia saa 4:30 asubuhi, mawaziri wote walikuwa tayari wameshaketi kwenye ukumbi wa mikutano wa Ikulu ilikofanyika shughuli hiyo ya kuwaapisha.
Kwenye meza kuu alikuwapo Makamu wa Rais, Samia Suluhu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Jaji Mkuu, Othman na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju na Naibu Spika, Tulia Ackson.
Dk. Magufuli aliingia ukumbini hapo saa 5:00 asubuhi na moja kwa moja akaanza kuwaapisha mawaziri hao shughuli iliyodumu kwa saa moja.
Baada ya mawaziri hao kula kiapo chao walitakiwa kwenda nje kupiga picha za ukumbusho na baada ya hapo kila mmoja alipanda gari lake na kuondoka.
Hali hiyo ni tofauti na ilivyozoeleka kwamba baada ya zoezi la picha, mawaziri hulakiwa kwa mbwembwe na shamra shamra na familia, ndugu, jamaa na marafiki wakipewa maua na kuvishwa mataji.
VITAFUNWA
Katika hatua nyingine, mara baada ya shughuli ya kuwaapisha mawaziri hao kumalizika, hakukuwa na vitafunwa kama ilivyozoeleka kwenye awamu ya JK.
Vinywaji pekee vilivyoonekana kwenye meza mbalimbali za Ikulu ni juisi, na hakukuwa hata na korosho.
Katika hafla ya uzinduzi wa Bunge la 11, Rais alikata Sh. milioni 230 katika bajeti ya siku hiyo na kuacha wabunge na wageni waalikwa wakinywa soda, juisi na korosho tu.
Kufurika kwa pombe na vinywaji vikali ilikuwa kawaida katika awamu iliyopita ya serikali, katika hafla hiyo.
Mawaziri hao waliingia Ikulu wakitumia magari binafsi lakini walipoondoka waliondoka na magari yaliyokuwa yameandaliwa kwa ajili yao.
Magari waliyoondoka nayo ni yale ambayo kwenye vibao vyake yamebandikwa herufi zinazowatambulisha mawaziri hao kama vile W-NJE, ikimaanisha Waziri wa Mambo ya Nje.
Nipashe ilipata taarifa kuwa baadhi ya mawaziri waliondoka Ikulu na kuelekea moja kwa moja kwenye wizara zao na kuanza kazi mara moja.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Charles Kitwanga aliondoka Ikulu na kuelekea moja kwa moja wizarani kwake ambako alipokelewa na Katibu Mkuu Mbarak Abduwakil na maofisa wengine wa wizara hiyo.
KIGWANGALA
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangalah, yeye ndiye aliwazidi kete mawaziri wenzake kwani alianza ziara ya ghafla akitokea kuapishwa Ikulu.
Kigwangala alitembelea ghafla hospitali ya Amana ambapo picha mbalimbali zinamwonyesha alikagua wodi mbalimbali za wagonjwa na kuzungumza na wagonjwa waliokuwa kwenye foleni.
Dk. Kigwangala aliongozana na mtu mmoja ambaye hakufahamika mara moja ambaye alionekana akichukua maelezo ya mazungumzo ya Naibu Waziri na wagonjwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene, naye alitinga wizarani kwake moja kwa moja akitokea Ikulu akifuatana na Naibu wake, Seleiman Jaffo, ilitaarifiwa Nipashe.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
No comments :
Post a Comment