Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, December 17, 2015

Mke amuua mume kwa kumpiga nondo kichwani


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi
By Phinias Bashaya, Mwananchi
Bukoba. Mkazi wa Kijiji cha Irogero, Kata ya Kamachumu wilayani Muleba, Archard Fredrick, anadaiwa kuuawa na mkewe kwa kupigwa na nondo kichwani akiwa amelala.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi alisema jana kuwa mtuhumiwa amelazwa Hospitali ya Ndorage akiwa chini ya ulinzi wa polisi kwa kosa la kujaribu kujiua kwa kunywa sumu baada ya tukio.
Ollomi alisema, mtuhumiwa aliuchukua mwili huo na kwenda kuufunika kwa majani ya migomba kwenye shamba lao jirani na nyumba yao.
“Uchunguzi wa awali unaonyesha chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi wa kifamilia,” alidai kamanda huyo.
Katika tukio lingine, Kamanda Ollomi alisema polisi wanamsaka mkazi mmoja wa Kijiji cha Nyaruzumbura, Tarafa ya Kaisho wilayani Kyerwa kwa tuhuma za kumuua mtoto wake kwa kumshmabulia kwa kumkata na panga kichwani.
Chanzo cha mauaji hayo inadaiwa kuwa ni ulevi wa pombe.
Mtoto huyo alifariki dunia alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Nkwenda.     

No comments :

Post a Comment