dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, December 15, 2015

Mradi wa gesi Mtwara-D’Salaam wakamilika


By Tausi Mbowe, Mwananchi
Dar es Salaam. Mradi wa kuchakata gesi asilia kutoka Madimba Mtwara-Songosongo hadi Dar es Salaam umekamilika na kuwezesha uzalishaji umeme katika mitambo ya Kinyerezi, Ubungo, Tegeta na kuingizwa kwenye gridi ya Taifa.
Kwa sasa mradi huo unazalisha asilimia 70 ya umeme wote unaotumika nchini kupitia Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC), Dk James Matagio alisema jana kuwa nchi inaelekea katika uchumi wa gesi kutoka katika uzalishaji wa umeme kwa kutumia mafuta na maji.
Alisema ujenzi wa bomba jipya la gesi umeongeza uzalishaji kwa asilimia 30.
Dk Matagio lisema mradi wa usambazaji gesi asilia katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Dar es Salaam pia unalenga kusambaza gesi katika nyumba 30,000 na magari 8,000.
Alisema upembuzi yakinifu na usanifu wa michoro umekamilika na kwa sasa wanatafuta fedha kutekeleza mradi unaotarajia kugharimu Dola 150 za Marekani.
Meneja wa Mawasiliano wa TPDC, Maria Msellemu alisema kutokana na ugunduzi wa mafuta nchini Uganda, Serikali ya nchi hiyo ilitia saini makubaliano na Tanzania kwa kushirikiana na TPDC na Kampuni ya Total.
Alisema makubaliano hayo yanalenga kuangalia uwezekano wa kusafirisha mafuta ghafi kutoka nchini humo kupitia Bandari ya Tanga hadi kwenye soko la nje.
“Tumeanzisha kampuni tanzu za Gaso ambayo inashughulikia gesi, Copec uagizaji wa mafuta na Kampuni ya International Business biashara za kimataifa,” alisema Msellemu.

No comments :

Post a Comment