Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, December 20, 2015

Muhongo: Bei ya umeme lazima ishuke

Image result for Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo,

Alitoa ahadi hiyo jijini Dar es Salaam jana wakati akizungumza masuala mbalimbali yanayohusu nishati ya umeme na namna wazawa wanavyoweza kuwekeza kuzalisha umeme.

Alisema idara na taasisi zilizo chini yake zinapaswa kukutana kutafuta majibu ya kudumu ya matatizo ya upatikanaji wa umeme wa uhakikia kwa sasa na kwa miaka 10 hadi 20 ijayo.

Alisema wafanyabiashara pamoja na wawekezaji  wa ndani wanakaribishwa kuwekeza katika sekta ya nishati.

Profesa Muhongo alisema Tanzani ina vyanzo vingi vya upatikanaji wa umeme, hivyo kwa yoyote ambaye anahitaji ni ruksa kuwekeza katika sekta hiyo ili kuongeza nishati hiyo.

“Kama nilivyowahi kusema huu umeme wa Megawati 1,400 hautoshi inabidi kuuongeza mara kumi ili  ifikapo 2025 tuwe nchi yenye kipato cha kati  kwa kuwa na umeme wa zaidi ya Megawati 10,000, kampuni ambazo zinaweza kuzalisha umeme wa Megawati 100, 200, 500, 1000… mnakaribishwa kuwekeza,” alisema.

Waziri huyo alisema wawekezaji hao wanatakiwa kuwekeza katika vyanzo mbalimbali vya kuzalisha umeme ikiwemo, gesi, makaa ya mawe, miradi mikubwa na midogo ya maji, nishati ya jua, upepo, jotoardhi, umeme wa mabaki ya taka, Bayogesi na Umeme wa mawimbi.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments :

Post a Comment