Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, December 18, 2015

Vigogo wa TRA kesi ya makontena nje

Kamishna wa Forodha na Ushuru wa TRA, Tiagi Masamaki na wenzake wawili waliachiwa huru kwa dhamana na Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam baada ya kutimiza masharti.
By James Magai, Mwananchi.
Dar es Salaam. Hatimaye vigogo watatu wa Mamlaka ya Mapato (TRA) wanaokabiliwa na kesi ya uhujujmu uchumi kutokana na sakata la upotevu wa makotena 329 kutoka bandari kavu ya Azam, wamerejea uraiani baada ya kuachiwa kwa dhamana.
Kesi hiyo iliyoko Mahakama ya Kisutu, inawakabili washitakiwa wanane lakini mawakili wa washtakiwa hao watatu, Majura Magafu na Alex Mgongolwa waliwasilisha maombi ya dhamana Mahakama Kuu, kwa kuwa Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.
Washtakiwa hao akiwemo Kamishna wa Forodha na Ushuru wa TRA, Tiagi Masamaki na wenzake wawili waliachiwa huru kwa dhamana na Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam baada ya kutimiza masharti.
Waliachiwa kwa dhamana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu Cyprian Mkeha, baada ya kuhakiki na kujiridhisha kuwa wametimiza masharti ya dhamana.
Mbali na Masamaki, washtakiwa wengine ambao waliomba dhamana na kupewa masharti hayo ambayo waliyatimiza jana ni meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja, Habibu Mponezya na meneja wa Udhibiti wa Forodha na Ufuatiliaji, Bulton Mponezya.
Washtakiwa hao watatu pamoja na wengine watano katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi wanadaiwa kuisababishia Serikali hasara ya Sh12.7 bilioni, kutokana na makontena hayo kuondolewa katika bandari hiyo bila kulipiwa kodi lakini wakadanganya kuwa yaliondolewa baada ya kulipa kodi hiyo.
Katika masharti ya dhamana yaliyotolewa na Jaji Winfrida Koroso, Desemba 15, walitakiwa kuwasilisha mahakamani pesa taslimu Sh2.16 biloni kila mmoja, au hati za mali zisizohamishika zenye thamani na kiasi hicho cha pesa.
Katika kutimiza sharti hilo, washtakiwa hao wote watatu kwa pamoja waliwasilisha mahakamani hapo jumla ya hati sita za mali zisizohamishika zilizoko Dar es Salaam, zote kwa pamoja zikiwa na thamani ya jumla ya Sh6.6 bilioni.
Masharti mengine ambayo washtakiwa hao walipewa na Mahakama Kuu na ambayo waliyatimiza jana ni pamoja kuwasilisha hati zao za kusafiria katika Mahakama ya Kisutu, kuwa na wadhamini wawili wanaotakiwa kuweka dhamana ya Sh20 milioni, ambao mmojawapo ni mtumishi wa umma.
Pia wanatakiwa kuripoti kwa Mkuu wa Upelelezi wa Polisi wa Mkoa kila baada ya majuma mawili, kutotoka nje ya jiji la Dar es Salaam bila idhini ya Mahakama ya Kisutu.

No comments :

Post a Comment