Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, December 17, 2015

Waziri Mwigulu aagiza wakulima wa korosho walipwe

Waziri wa Kilimo Uvuvi na Mifugo, Mwigulu Nchemba.
Waziri wa Kilimo Uvuvi na Mifugo, Mwigulu Nchemba, amemwagiza  mnunuzi wa zao la korosho, Kampuni ya Sparkle Way Limited ya jijini Dar es Salam, kuhakikisha hadi ifikapo Desemba 21, mwaka huu iwe imewalipa wakulima wa Mkoa wa Pwani fedha wanazodai kiasi cha Sh. bilioni 3.4.
 
Waziri huyo alitoa agizo hilo jana katika kikao cha wadau wa korosho Mkoa wa Pwani kilicholenga kujadili mnada wa tano wa korosho ambao fedha zake hazijawafikia wakulima hadi sasa.
 
Waziri Nchemba alilazimika kutoa kauli hiyo kufuatia kusuasua kwa malipo ya fedha za wakulima kutoka kwa kampuni hiyo ambayo kwa mujibu wa kanuni na sheria za manunuzi ya  korosho alitakiwa kufanya malipo hayo Desemba 4, mwaka huu.
 
Mnunuzi huyo ametakiwa kuingiza fedha leo Desemba 17, kwenye akaunti ambayo ataelekezwa na Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Pwani (Corecu) ili ifikapo Jumatatu wakulima wa zao hilo waanze kulipwa fedha zao.
 
“Habari ya kucheza na watu wasio na sauti gharama yake ni kubwa sana, hii si sahihi, mnachopaswa kufanya wanunuzi wote ni kutofanya kila kitu kwa mazoea,” alisema waziri huyo.Akitoa sababu za kuchelewesha malipo ya korosho zaidi ya tani 500, mwakilishi wa kampuni hiyo, Salum Mkemi, alisema alihitaji zikapimwe tena ubora wake ili kuepusha hasara ambayo aliipata mwanzo.
 
Mkemi alidai awali alinunua korosho kwenye minada iliyopita lakini zilipofika India zilikuwa zimeanza kuota, hivyo kusababisha hasara ya tani 100 yenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 200.
 
Akifafanua zaidi alisema walishindwa kulipa  mapema kutokana na hasara waliyoipata awali, lakini hadi kufikia tarehe hiyo waliyoagizwa watahakikisha wanawalipa wakulima hao.
 
Alisema ukosefu wa ghala la serikali la mkoa kumesababisha kuchangia kwa hujuma zinazofanyika kwenye maghala ya korosho na ndicho chanzo cha kuwapo kwa korosho ambazo si za kiwango kinachotakiwa.
 
Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo, alisema tangu kuanza kwa stakabadhi ghalani minada minne ilienda vizuri isipokua mnada wa tano ambao fedha zake zilikua hazijalipwa.
 
Ndikilo aliitaka Bodi ya Korosho pamoja na viongozi wa ushirika kufanyia kazi malalamiko yaliyotolewa ili kuondoa vikwazo katika biashara hiyo.
Katika mnada huo, kiasi cha Sh. bilioni 3.7 zilitarajiwa kukusanywa na malipo kufanyika kwa wakulima wa korosho.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment