dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, January 18, 2016

Gazeti Mawio wamshangaa Nape kuwafutia usajili

Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Sanaa, Nape Nnauye.
Viongozi wa kampuni ya Victoria Media inayomiliki gazeti la Mawio wameelezea kusikitishwa kwao na uamuzi wa serikali wa kulifuta gazeti hilo huku wakidai kushangazwa na uamuzi huo mzito uliotangazwa jana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Sanaa, Nape Nnauye.
 
Akizungumza na Nipashe jana, Mkurugenzi wa kampuni hiyo ambaye pia ndiye aliyekuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la Mawio lililokuwa likitoka kila wiki, Simon Mkina, alisema wameshItushwa na uamuzi wa kufutwa kwa gazeti hilo na kwamba, pamoja na hatua hiyo kali dhidi yao, kinachowashangaza ni ukweli kuwa hadi sasa hawajapata taarifa yoyote rasmi ya serikali kuwaarifu jambo hilo ili wajue ni hatua gani wachukue.
 
“Sisi (Mawio) ndiyo waathirika wakubwa wa taarifa hii. Kinachotushangaza ni kuwa hadi sasa hatujapata barua yoyote ya serikali kuhusiana na jambo hili. Nasi tumemsikia tu Waziri (Nape) akitangaza kutufuta na kwakweli tumeshtushwa sana. Tutakaa na kuamua ni hatua gani tuchukue kutokana na uamuzi huu,” alisema Mkina wakati akizungumza na Nipashe jana.Kadhalika, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa kampuni hiyo, Yusuf Abood, alisema hadi jana uongozi wa kampuni ya yao (Victoria Media) ulikuwa haujapata barua yoyote ya kufutwa kwa gazeti hilo bali wanasikia kupitia katika mitandao ya kijamii na vyombo vingine vya habari.
 
Alisema serikali inapaswa kutoa sababu zilizosababisha kufutwa kwa gazeti hilo kwa maandishi kwani kuna adhabu za kulifuta gazeti na adhabu za kulifungia gazeti.
 
Alisema kulifuta gazeti la Mawio kutakuwa kumeminya haki ya wananchi ya kupata habari na pia kuwanyima wananchi haki ya kupata taarifa.
 
Akieleza zaidi, alisema uongozi wa kampuni ya Victoria Media ulikuwa ukipokea barua kila baada ya wiki mbili kutoka serikalini iliyokuwa inawataka kujieleza au kutoa maelezo kuhusu habari fulani na hivyo, hadi kufutwa kwa gazeti hilo,  uongozi wao bado haujafahamu ni habari gani iliyosababisha gazeti lao kufutwa.
 
NAPE ASIMULIA KISA MAWIO KUFUTWA   
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Nape alisema Serikali imelazimika kulifuta gazeti la Mawio kutoka katika orodha ya magazeti yaliyopo nchini kutokana na kukithiri kwake katika kutoa habari zisizozingatia miiko ya uandishi wa habari licha ya kuwahi kuonywa mara kadhaa katika kipindi cha takribani miaka nane.
 
Alisema amri ya kulifuta gazeti hilo imetolewa katika tangazo la Serikali namba 55 la Januari, mwaka huu, kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti Sura ya 229, kifungu cha 25(1).
 
Nape alisema mojawapo ya habari zilizosababisha gazeti hilo kufungiwa ni pamoja na ile iliyokuwa na kichwa cha habari “Machafuko yaja Zanzibar” pamoja na ile ya “Seif Rais Zanzibar, maandalizi ya kumtangaza yaiva.”
 
Alisema hatu hiyo inalizuia gazeti hilo kuchapishwa katika njia nyingine yoyote ikiwa ni pamoja na mitandao kwa mujibu wa Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta, Sura ya 306.
 
“Serikali kwa masikitiko makubwa imechukua uamuzi huu kutokana na mwenendo wa uandishi wa gazeti hilo usioridhisha na kuandika na kuchapisha habari zenye mwelekeo wa uchochezi na pia kuhatarisha amani, utulivu na usalama wa nchi,” alisema Nape.
 
Alieleza kuwa serikali haikukurupuka kulifuta gazeti hilo, kwani Msajili wa Magazeti amekuwa akifanya juhudi kubwa na za muda mrefu kuanzia Juni, 2013 hadi Januari 2016, kwa kumtaka Mhariri wa gazeti hilo kubadili aina ya uandishi wa habari na makala bila ya mafanikio.
 
Alisema Msajili wa Magazeti aliwahi kufanya mawasiliano na  Mhariri wa gazeti hilo mara nane lakini mhariri wa gazeti hilo hakuzingatia ushauri mzuri aliopewa.
 
MABANGO YA UCHOCHEZI
Kuhusu washiriki waliobeba mabango ya uchochezi katika sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Zanzibar yaliyofanyika Januari 12, mwaka huu, Nape alisema wahusika hao wanashughulikiwa, lakini hakutaka kulizungumzia suala hilo kiundani kwa madai kuwa halikuwa suala la kihabari
 
Nape alitoa wito kwa wamiliki, wahariri, waandishi na watangazaji wa habari kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za taaluma ya uandishi wa habari ambazo zikizingatiwa hakutakuwa na migogoro yoyote.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment