dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, January 18, 2016

Matokeo kidato cha pili yaibua mapya

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako.
Shirikisho la Wamiliki na Mameneja wa Shule na Vyuo visivyo vya Serikali Tanzania (Tamongsco) limelijia juu Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) kwa kutangaza matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha pili kwa kutumia mfumo wa GPA ambao umekuwa ukilalamikiwa na wadau wa elimu nchini.
 
Aidha, shirikisho hilo limesema Necta imekiuka sheria ya 107(3) (4) kwa kutangaza matokeo ya mtihani huo bila kushirikisha Tamongsco kama sheria inavyoelekeza.
 
Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Benjamin Nkonya, alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu Mfumo wa Wastani wa Madaraja ya Ufaulu (GPA).
 
Alisema shirikisho hilo limesikitishwa kuona matokeo ya mtihani wa kidato cha pili uliofanyika mwaka jana yakitangazwa kwa kutumia mfumo wa GPA kabla ya hoja walizoziwasilisha kwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako, hazijapatiwa ufumbuzi.“Januari 6, 2016 wanachama wa Tamongsco tulikutana na Waziri wa Elimu na tukawasilisha hoja zetu tano kuhusu mfumo wa GPA na tukamshauri asitishe mfumo huu mpaka pale hoja hizo zitakapojibiwa,” alisema.
 
Nkonya alisema hatua ya Necta kuendelea kung’angania kutumia mfumo huo katika kutangaza matokeo inawawia vigumu wadau wa elimu kufanya tathimini ya wanafunzi katika mazingira ambayo hawawezi kufafanua utaratibu unaotumika katika upangaji wa matokeo ya watahiniwa.
 
Alisema pamoja na kwamba matokeo ya mtihani huo yanaonyesha shule zisizo za serikali zimeongoza, lakini Tamongsco haiwezi kusema kama matokeo hayo ni ya kujivunia kwa kuwa haielewi vizuri mfumo wa GPA unavyofanya kazi.
 
“Kinachosikitisha ni kwamba somo la kiingereza ambalo ndilo linalotumika kama lugha ya kufundishia limo katika orodha ya masomo ambayo wanafunzi wamefanya vibaya zaidi na hivyo kuzua maswali inakuweje mwanafunzi afanye vizuri katika masomo wakati lugha inayotumika kumfundishia haielewi,” alisema na kuongeza:
 
“Kinachotusikisha ni kuona kwamba baadhi ya watahiniwa wanaonekana kufaulu kwa mfumo wa GPA, lakini wakifika ngazi ya elimu ya elimu huonekana hawafai, wanapoingia katika soko la ajira wanapata changamoto kubwa kupata ajira.”
 
Katibu Mtendaji wa Necha, Dk. Charles Msonde, alipotafutwa na Nipashe kwa njia ya simu ili kuzungumzia suala hilo, alipokea simu yake na kisha kuikata na kutuma ujumbe mfupi wa maneno (sms) kwamba muda huo hawezi kuongea chochote.
 
Baadaye alipotumiwa swali kwa ujumbe mfupi wa maneno (sms) hakujibu.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment