Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, January 16, 2016

'Mgonjwa wa Magufuli' afungwa Muhimbili

Rais Dk. John Magufuli.
Chacha Makenge (39), ambaye ni maarufu kwa jina la ‘mgonjwa wa Magufuli’ ameondolewa wodini kwenye Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), jijini Dar es Salaam, na kupelekwa wodi ya magonjwa ya akili kwa nguvu, kwa kutumia amri ya mahakama.
 
Kuwekwa wodi ya magonjwa kwa amri ya mahakama ni moja ya aina ya hukumu za mhimili huo wa dola.
 
Zoezi hilo la kumhamisha lilifanyika juzi saa 6.30 mchana ambapo uongozi huo ulimpeleka katika kitengo cha magonjwa ya akili kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi kutokana na vitendo vyake kutokuwa vya kawaida.
 
Akizungumza na Nipashe jana, Ofisa Ustawi wa Jamii wa MOI. Frank Matua, alisema walichukua hatua hiyo baada ya Makenge kugoma kuondoka wodini mara kadhaa licha ya kuruhusiwa na madaktari baada ya afya yake kuwa nzuri.Makenge alilazwa wodi ya Sewahaji namba 18 na kitanda chake kilikuwa cha tatu mstari wa kwanza, upande wa kushoto unapoingia wodini.
 
Alisema baada ya kuona mgonjwa huyo anaendelea kung’ang’ania wodi na kukaidi maelekezo ya madaktari, waliamua kwenda mahakamani kuomba kibali cha kumuondoa kwa nguvu kwenda kumpima akili.
 
“Tumemuondoa kwa kutumia amri ya mahakama na kumpeleka kitengo cha magonjwa ya akili, kule ana faili lake la siku nyingi," alisema Mutua na kueleza, "sasa MOI haitawajibika na Makenge kama ilivyokuwa huko nyuma.
 
"Ametusumbua hapa kwa muda mrefu sana ingawa tumepata shida kumuondoa, lakini tumefanikiwa.”
 
Alisema Makenge aliwapa changamoto nyingi kwani awali alipopelekwa katika kitengo cha magonjwa ya akili, siku ya pili alitoroka na kurudi Moi.
 
“Tunaamini mgonjwa wetu alikuwa na matatizo ya akili na ndiyo maana tukachukua hatua ya kushirikiana na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kumchunguza,” aliongeza kusema.
 
Novemba 9 mwaka huu wakati Rais Dk. John Magufuli, alipofanya ziara ya ghafla katika Hospitali ya Muhimbili, alikutana na Makenge ambaye alimwelezea matatizo mbalimbali wanayokabiliana nayo wagonjwa na hasa kuharibika kwa mashine za CT-Scan na MRI.
 
Rais Magufuli baada ya kupewa taarifa hizo na Mekenge, aliamuru mgonjwa huyo atibiwe kwa gharama zake hali ambayo ilisababisha watu wamwite mgonjwa wa Magufuli.
 
Mgonjwa huyo amekuwa na vituko vingi tangu awasili hospitalini hapo mwaka jana ambapo Kaimu Mkurugenzi wa Tiba kwenye taasisi hiyo, Samuel Swai, alisema Makenge amekuwa msumbufu kiasi ambacho madaktari wameshauri kufanya utafiti zaidi kuhusu matatizo mengine.
 
"Sisi madaktari baada ya kumfanyia vipimo vyote na kumtibu ugonjwa uliokuwa ukimsumbua, tumejiridhisha hana tena matatizo yaliyomsumbua nyuma ya mgongo lakini cha ajabu hataki kuondoka," alisema Swai.
 
Mkurugenzi huyo alieleza kuwa kwa muda mrefu Chacha amekuwa na vituko vingi kwenye wodi aliyolazwa, ikiwa pamoja na kukataa kulala kitandani na badala yake amekuwa akilala chini hali ambayo iliwalazimu kuanza mchakato wa kupima akili yake.
 
CHANZO: THE GUARDIAN

No comments :

Post a Comment