Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, January 16, 2016

Wakurugenzi watatu wapya washindwa kasi Bandari.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Pangua Pangua imeendelea kuwakumba vigogo wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), ambapo safari hii wakuu wa vitengo vitatu ambao waliteuliwa hivi karibuni kufuatia tuhuma za ufisadi, wameondolewa na kurejeshwa wizarani kusubiri majukumu mengine baada kile kilichoelezwa kuwa wameshindwa kwenda na kasi iliyokuwa inatakiwa.
 
Vigogo hao waliong’olewa jana TPA, ni aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Tehama, Peter Gaule, Mkuu wa Utawala na Rasilimali Watu, Kilian Chale, na Kaimu Mkurugenzi wa Manunuzi, Mashaka Kasanza.
 
Waziri wa  Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, ndiye aliyetangaza kuondolewa kwa watumishi hao jana wakati akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
 
Waziri Mbarawa alisema nafasi ya Ofisa Manunuzi Mkuu itashikiliwa na Benito Kalinga kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Meneja Rasiliamali Watu itakaimiwa na Antony Mbilinyi wa TCRA wakati Mkuu wa Tehama atakuwa Abrahaman Mbawa, kutoka wizarani.“Tumefanya mabadiliko ya ghafla baada ya kuona utendaji kazi wao haukuwa mzuri katika sehemu zao za kazi, hivyo watabaki wizarani kusubiri kama itatokea nafasi basi watapewa, lakini hawa niliowateua leo (jana), nao nitaendela kuchunguza mienendo yao ya kazi kama inaridhisha,” alisema Profesa Mbarawa.
 
Waziri alisema uteuzi huo unaweza kuleta mabadiliko katika bandari hiyo pamoja na kuinua uchumi wa taifa kwa sababu wakuu hao wa vitengo walioondolewa walishindwa kuhimili majukumu waliyopewa ndani ya  TPA.
 
Watumishi hao waliong’olewa ni wale waliotolewa Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi kwenda kuziba mapengo ya wafanyakazi waliotimuliwa TPA wakati wa mtikisiko wa serikali ya awamu ya tano ilipobaini wizi na ukwepaji kodi.
 
Mtikisiko ndani ya TPA ulianza mwishoni mwa mwaka jana baada ya Rais John Magufuli kubaini mianya ya ukwepaji wa kodi hivyo kulazimika kuchukua hatua kali ikiwemo kuwasimamisha kazi vigogo kadhaa wa mamlaka hiyo na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA).
 
WALIOSIMAMISHWA KAZI
Miongoni mwa vigogo ambao walianza kuonja chungu ya serikali ya Rais Magufuli ni aliyekuwa Meneja wa Bandari Awadh Masawe.
Wafanyakazi kadhaa wa TPA pia wanashikiliwa na polisi kuhusina na ama utoroshaji wa makontena 11,000 bila kulipiwa tozo ya bandari (wharfage charges), ama makotena zaidi ya 2,800 bila kulipiwa kodi.
 
Aidha, Kamishna Mkuu wa Mamalaka ya Mapato Nchini (TRA), Rashed Badi aliyesimamishwa kazi pamoja na vigogo wengine saba waliokamatwa na polisi akiwemo Kaimu Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa, Tiagi Masamaki, kutokana na kutolewa kwa makontena 329 bila kulipiwa ushuru.
 
Katika sakata hilo zaidi ya wafanyakazi 40 wa TRA walishikiliwa na Jeshi la Polisi kuhusina na tuhuma hizo ambazo zimeisababishia serikali hasara ya mabilioni ambapo pia Magufuli alivunja Bodi ya Mamlaka ya Bandari.
 
Mbali na kuvunja bodi hiyo, pia alitengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Mhandisi Profesa Joseph Msambichaka na kumsimamisha kazi Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Shaaban Mwinjaka kwa kushindwa kusimamia utendaji wa TRL na TPA.
 
Wengine waliokwisha kumbana na rungu la Rais Magufuli ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa  Takukuru, Dk. Edward Hoseah, ambaye ilielezwa kuwa Rais hakuridhishwa namna taasisi yake ikitekeleza majukumu na kushindwa kukabiliana na vitendo vya rushwa hususani kwenye upotevu wa mapato ya serikali katika bandari ya Dar es Salaam. 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment