Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, February 12, 2016

Majaliwa, Lukuvi wang’ara utafiti

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (Kushoto) na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuv (Kulia)
By Suzan Mwillo, Mwananchi 
Dar es Salaam. Asilimia 90.2 ya Watanzania wanakubali uamuzi wa Rais kumteua Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu, huku William Lukuvi akiibuka kuwa waziri anayekubalika kuliko wote, kwa mujibu wa utafiti.
Utafiti huo uliofanywa na kampuni ya InfoTrak na Midas Touche East Africa Ltd kwa ufadhili wa kampuni ya Mwananchi Communications, ulihusisha watu 1,200 wa Bara na Zanzibar waliohojiwa kati ya Februari Mosi na 7.
Kwa mujibu wa utafiti huo, asilimia 86.9 ya wakazi wa vijijini waliohojiwa kama wanakubali uteuzi wa Waziri Majaliwa, walimkubali mbunge huyo wa Ruangwa kushika nafasi hiyo ya mtendaji mkuu wa Serikali, wakati asilimia 86.9 ya wakazi wa mjini pia walionyesha kuafiki.
Kutokana na usiri wa Rais John Magufuli, hakuna aliyetarajia Majaliwa kupewa nafasi hiyo nyeti, lakini tangu aanze kazi amekuwa akifuatilia kwa karibu ukwepaji kodi kwenye Bandari ya Dar es Salaam na kufichua ufisadi mkubwa.
Doa lake kubwa lilikuwa ni kutangaza kuzuia mikutano na wanasiasa walioshindwa kwenye Uchaguzi Mkuu, lakini alilisafisha wiki iliyopita bungeni alipofafanua kuwa lilihusu jimbo lake la Ruangwa tu.
Kwa mujibu wa utafiti huo, kati ya waliohojiwa asilimia 91.3 ya wanawake walimkubali wakati wanaume ni asilimia 89.2.
Katika mgawanyiko wa kanda, wananchi wa Kanda ya Kati walisema wanakubali uteuzi huo kwa asilimia 99.3, Pwani asilimia 87, Kanda ya Ziwa asilimia 89.6, Kanda ya Kaskazini asilimia 89, Kusini 90.7 na Zanzibar 94.2
Walipoulizwa kuhusu kuridhishwa na uteuzi wa Baraza la Mawaziri, asilimia 90.2 ya wananchi wa Kanda ya Kati walisema ndiyo, Pwani asilimia 77.4, Kanda ya Ziwa asilimia 83.1, Kanda ya Kaskazini asilimia 77.2, Kusini asilimia 76.6 na Zanzibar asilimia 84.1.
Asilimia 83.6 waliosema ndiyo ni wakazi wa vijijini na asilimia asilimia 74.0 ni wakazi wa mjini huku wanawake wakionyesha kulikubali baraza hilo kwa asilimia 82.6 na wanaume asilimia 78.6. Walipoulizwa kuhusu kuliamini baraza hilo, asilimia 43 walisema wana imani nalo sana, asilimia 36.5 wana imani nalo kiasi, asilimia 15.6 wana imani nalo kidogo na asilimia 4.9 hawana imani nalo kabisa, huku asilimia 81.6 wakisema baraza hilo ni dogo jambo ambalo ni zuri na asilimia 18.4 wakisema ni kubwa jambo ambalo si zuri.
Kuhusu utendaji wa baraza, Lukuvi, ambaye ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, aliibuka kidedea kwa kupata asilimia 13.1, akifuatiwa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako aliyepata asilimia 11.4
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alipata asilimia 10.2, Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jummane Maghembe ( 8.3), Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (7.1), Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (6.8), Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (5.9), Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango asilimia 4.1.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (3.8), Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene (3.7), Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba (3.7), Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Gerson Lwenge (3.7).     

No comments :

Post a Comment