Inasemekana karibu wagonjwa kutoka sehemu mbali mbali sio za Zanzibar tu bali za Tanzania nzima sasa wataanza kukimbilia kwenye hospitali ya Mkoani, Pemba, hospitali ambayo ni ya kisasa zaidi na inategemewa kufunguliwa muda si mrefu na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).
Wananchi wa Pemba watanufaika sana na huduma zitakazotolewa katika hospitali hii. Aina ya hospitali kama hii kwa Zanzibar haijawahi kujengwa, kwani muonekano wa majengo yake ni ya kipekee.
Zaidi ya matibabu ya kawaida yatakayopatikana, patakuwepo pia upasuaji, matatizo ya ubongo, CitiScan, X-ray, huduma za mama wajawazito ikiwemo mashine ya watoto njiti na huduma nyenginezo za kisasa zitapatikana pia.
Hii itakuwa ni hospitali ya pili katika visiwa vya Zanzibar kuwa na CitiScan. Ya kwanza ni ile iliyopo Unguja ijulikanayo kwa jina la TASAKHTAA HOSPITAL iliyopo ubavuni wa Mnazi Mmoja Hospital. Hii inamilikiwa na Mfanya biashara maarufu Zanzibar Bwana Salim Turkey iliofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein katika mwisho wa mwezi wa March, 2015 - for more details about Tasakhtaa Hospital click here:
(http://zanzibarnikwetu.blogspot.ca/2015/03/zanzibar-gets-modern-hospital-hakuna.html#more).
TUJIKUMBUSHE KUHUSU ABDALLA MZEE HOSPITAL:
http://zanzibarnikwetu.blogspot.ca/2016/02/balozi-seif-akagua-maendeleo-ya-ujenzi.html
Na Muandishi wa ZNK, Zanzibar.
Na Muandishi wa ZNK, Zanzibar.
No comments :
Post a Comment