Wananchi kisiwani Pemba, wametakiwa kuhudhuria kwa wingi katika ufunguzi wa hospitali mpya ya Abdalla Mzee Mkoani inayotarajiwa kufunguliwa rasmi tarehe 26 mwezi huu.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini pemba Mhe.Mwanajuma Majid Abdalla,wakati alipokuwa akizungumza na maafisa wadhamini wa wizara zote za serikali na watendaji wa taasisi nyegine hapo katika hospitali ya Abdalla Mzee mkoani.
Amesma kuwa lengo la kuitisha mkutano huo nikuzungumzia maandalizi ya ufunguzi wa hospitali hiyo unatarajiwa kufunyika wiki ijahyo ya mwezi huu ambapo mgeni rasmi anatarajiwa katika ufunguzi huo ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Muhamed Shein.Aidha amewataka maafisa wadhamini hao kuhakikisha kwamba kila alopangiwa dhamana ndani ya ofisi yake ahakikishe anatekeleza wajibu wake.
Nae Mkuu wa Wilaya Mkoani Ndg Hemed Suleiman Abdalla, ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwajengea wananchi wake hospitali ya rufaa kisiwani pemba hivyo hapana budi wananchi hao kuhudhuria kwa wingi siku ya ufunguzi kwani ni jambo la historia kubwa na la kujivunia kupata kitu hicho kwao.
Hata hivyo amemuoba afisa mdhami wa shirika la umeme pemba kuhakikisha kipindi hiki cha matayarisho ya ufunguzi wa hospitali umeme uwepo muda wote pamoja na kuongeza bidii za kukamilisha ukarabati wao ili kuweza kupata umeme wa uhakika .
Kwa upande wake mkurugenzi wa wizara afya Zanzibar Mohd Dahoma amesema kwamba maandalizi yako hatua mzuri hivyo amewahimiza wananchi kuungana nao ili kuona wanasherehekea ufunguzi huo wa hospitali hiyo mpya ya kisasa.
No comments :
Post a Comment