Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, February 18, 2017

Sasa ni mtafutano wa Jeshi la Polisi na Mbowe!



Jeshi la Polisi kanda maalum Dsm limemtaka m/kiti wa chama cha Demokrasia na maendeleo chadema kujisalimisha Polisi mara moja kwa ajili ya mahojiano yanahusuhu vita dhidi ya dawa za kulevya baada juhudi za kumsaka katika makazi yake kushindikana huku simu yake ya mkononi ikiwa imezimwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini DSM Kamanda wa Polisi kanda maalum DSM Kamishna Simon Siro amesema bw,mbowe aliahidi kwenda mwenyewe juzi tar 15,lakini hakwenda lakini jeshi hilo lilimtafuta usiku na mchana katika makazi yake na kumpigia simu lakini simu yake ilizimwa .

Aidha jeshi hilo limesema watuhumiwa watatu Agnes Masogange,Rashid Iddi au Chid Mapenzi na Wallis Latif Nasher ambae ni muuza magari katika eneo la mikocheni watapandishwa kizimbani jumatatu kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya lakini pia walibainika wanatumia dawa hizo baada ya kupelekwa kwa mkemia mkuu.

Katika kupambana na askari feki jeshi hilo limemtia mbaroni aliyekuwa askari magereza wa cheo cha kopro Peter Elias Msigwa aliyekuwa mtumishi katika gereza la keko,ambaye alifukuzwa kazi dec mwaka jana,lakini alikamatwa jana akiwa na mavazi ya kiaskari tena akiwa amejipandisha cheo kutoka Copro hadi sajenti wa Polisi.

Jeshi hilo pia limesema limewatia mbaroni watu 65 kwa makosa ya kukutwa na dawa za kulevya pamoja na watuhumiwa 73 wa wizi na ujambazi wa kutumia silaha ,mitambo mitano ya Gongo,lita 270 pamoja na Puli 250 za bangi.

No comments :

Post a Comment