Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Jonathan Lema akiwa kwenye gari baada ya kuachiwa kwa dhamana leo.
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema) Godbless Lema, ameachiwa kwa dhamana leo katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.
Lema ameachiwa kwa dhamana ikiwa ni takribani miezi minne tangu awekwe rumande kwa kesi ya uchochezi.
Polisi wa kutuliza ghasia walijaa mahakamani hapo wakiwafukuza wafuasi wa Lema waliojaa katika viwanja vya mahakama hiyo.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe walikuwepo mahakamani hapo leo.
Kabla ya hukumu ya leo: Lowassa, Sumaye Wawasili Mahakamani Kusikiliza kesi ya Lema
Viongozi mbalimbali wa Chadema wakiongozwa Katibu Mkuu wa Chadema Dr Vicent Mashinji, Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Edward Lowasa, Waziri Mkuu Msaatafu Sumaye na Meya wa Jiji la Arusha Mjini Kalisti Lazaro wakiwa mahakamani kusikiliza uamuzi wa Mahakama kuhusu dhamana ya Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema unaotolewa leo
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema akishuka kwenye gari kuingia mahakamani.




No comments :
Post a Comment