zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, March 3, 2017

ZANZIBAR: Mihadarati yamliza Mwakilishi

MWAKILISHI wa Viti Maalum katika Baraza la Wawakilishi kutoka Pemba, Zulfa Mmanga, ameangua kilio ndani ya baraza hilo wakati akichangia hoja binafsi ya ongezeko la uingizaji na utumiaji wa dawa za kulevya.

Hoja hiyo binafsi, iliwasilishwa katika Baraza la Wawakilishi jana na Mwakilishi wa Jimbo la Mpendae, Mohammed Said Dimwa.
Akiwasilisha hoja hiyo, Dimwa alisema kuwa kwa mwaka 2016, bado kuna ongezeko la kesi za dawa za kulevya Zanzibar kulinganisha na miaka ya nyuma.

Kwa mujibu wa Mwakilishi huyo, jumla ya kesi 170 za dawa za kulevya zilifunguliwa mwaka jana.

Alisema pamoja na jitihada kubwa zinazochukuliwa na nchi mbalimbali kupiga vita biashara haramu ya dawa za kulevya, lakini nchi nyingi katika Bara la Afrika ikiwamo Zanzibar, zinaendelea kupata changamoto kubwa inayotokana na uzalishaji, utengenezaji, usafirishaji na matumizi ya dawa za kulevya.
Akichangia hoja hiyo huku akibubujikwa na machozi, Zulfa alisema vijana wengi Zanzibar wameathirika kutokana na dawa za kulevya na kutolea mfano wa ndugu yake wa kuzaliwa tumbo moja aliyekumbwa na tatizo hilo.

Alisema Zanzibar ina sheria nzuri ya kupambana na dawa za kulevya, lakini tatizo hilo limekuwa likiongezeka.
"Hii inaonyesha kuwa Jeshi la Polisi limeshindwa kupambana na dawa za kulevya," alisema Mwakilishi huyo.

“Mimi nina uchungu na dawa za kulevya kwa sababu ndugu yangu wa damu ambaye ni pekee wa kiume katika familia yangu, ameshaathirika na dawa za kulevya licha ya kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi kuhusu watu tunaowatuhumu kufanya biashara hii, lakini hakuna hatua zilizochukuliwa,” alisema Zulfa huku akiangua kilio na kusitisha kuchangia hoja hiyo baada ya kuunga mkono.

Mwakilishi mwingine wa Viti Maalum, Mtumwa Suleiman Makame, ambaye naye pia mtoto wake ameathirika na dawa za kulevya, aliitaka serikali kupambana na vijiwe vya vijana wanaojihusisha na dawa hizo kwa kuwa vinafahamika.

Aidha, Makame aliitaka serikali kuzifanyia ukaguzi wa mara kwa mara hoteli za kitalii zinazotuhumiwa kuhusika na dawa za kulevya hasa katika ukanda wa Nungwi na Kiwengwa Unguja.

“Sisi wanawake tuna uchungu sana na watoto wetu, kwa hiyo tunaitaka serikali kupambana kikamilifu na matumizi ya dawa za kulevya kwa kutumia vyombo vyake vya ulinzi likiwamo Jeshi la Polisi,”alisizitiza Mwakilishi huyo.

Naye Mwakilishi Mwantatu Mbaraka, alisema tatizo la matumizi ya dawa za kulevya halitokani na ukosefu wa ajira kwani imabainika kuwa wengi wa watumiaji hao, ni wanafunzi wa shue za msingi na sekondari.

Mewantatu alisema wakati umefika jamii wakiwamo vijana, kupewa elimu kuhusiana na athari za dawa za kulevya ili kuepuka wimbi la nguvu kazi ya taifa kupotea.

“Tunaweza kupambana na tatizo la dawa za kulevya, lakini kwanza jamii ipewe elimu kuhusu athari ya dawa za kulevya na ni vyema elimu hiyo ikaanza shuleni kwa kuwa hali ni mbaya kwa wanafunzi,” alisema mwakilishi huyo.

No comments :

Post a Comment