Mbunge wa Misungwi (CCM), Charles Kitwanga
Dar es Salaam. Licha ya Mbunge wa Misungwi (CCM), Charles Kitwanga kupewa majibu makali na Waziri wa Maji, Gerson Lwenge hivi karibuni bungeni Dodoma ikiwamo kuhama chama, ameibuka akisema yale aliyochangia kwenye bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji ni kama ni ali-‘beep’ na kwamba mazito yanakuja.
Waziri huyo wa zamani wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kitwanga, wakati akichangia mjadala wa bajeti hiyo alitishia kuwahamashisha wananchi 10,000 wa jimbo lake kwenda kuzima mtambo wa maji wa Kijiji cha Ihelele kutokana na kijiji hicho kutopata maji katika chanzo hicho.
Lakini Waziri Lwenge akijibu hoja hizo aliifananisha nia hiyo ya Kitwanga na uasi na kuonyesha kama hathamini kazi inayofanywa na chama chake hivyo kumtaka ahame kama haridhiki.Ingawa jana Kitwanga hakuwa tayari kutaja mambo hayo mazito, amesisitiza kuwa hivi sasa yeye ni mbunge hivyo anatekeleza wajibu wake kisheria wa kuwawakilisha wananchi Misungwi mkoani Mwanza.
Kitwanga amesema kuna vitu viwili watu wanashindwa kuelewa kuwa yeye alikuwa naibu waziri kisha waziri kamili, hivyo kuna mambo kutokana na sheria za utumishi wa umma alishindwa kuyasema lakini hivi sasa ni mbunge.
“Sasa hivi mimi ni mbunge, nina wajibu wa kuhoji. Nawaambia siku ile nili- ‘beep’, sasa nitapiga zaidi. Wananitambua nilivyokuwa kijana nilikuwa mwanaharakati lakini sasa hivi ndiyo uharakati umezidi,” amesema Kitwanga.
No comments :
Post a Comment