Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiagana na Mjumbe wa Baraza la Mainduzi ambae pia ni Waziri asiye na Wizara Maalum Mh. Said Soud Said kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume akiondoka kupitia Dar es salaam kwa safari ya kuhudhuria Tamasha la Uchumi la Dunia { World Economy }linalotarajiwa kufanyika Amman Nchini Jordan.
Balozi Seif akiagana na Viongozi mbali wa Serikali na Taasisi za Umma kuelekea Nchini Jordan kwenye kumuakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufili kwenyeTamasha hilo la siku Tatu linaloanza Tarehe 19 Mei 2017.
Balozi Seif akisalimiana na Wahudumu wa Ndege ya Tropical akijiandaa kuanda kupitia Mjini Dar es salaam kwa safari ya Mjini Amman Nchini Jordan akiambatana na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Balozi Amina Salum Ali na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameondoka Zanzibar kupitia Mjini Dar es salaamu kuelekea Amman Nchini Jordan kuhudhuria Jukwaa la Uchumi la Dunia { World Economy Forum - WCF} la Siku Tatu litakalohudhuriwa na zaidi ya Wajumbe 2,000 kutoka Nchi 58 Duniani.
Balozi Seif anamuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kwenye Jukwaa hilo la Kanda ya Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika litakaloshirikisha Vingozi Wakuu wa Nchi, Wafanyabiashara,wamiliki wa Makampunni ya Kimataifa, Wawakilishi wa Taasisi za Kiraia, Mashirikia ya Kimataifa, Wana Habari pamoja na Vijana.
Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefuatana na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi ameagwa na Mwaziri, baadhi ya Watendaji Wakuu wa Serikali pamoja na Viongozi wa Kisiasa.
Katika Mkutano huo wa Jukwaa la Dunia la Uchumi Balozi Seif ameongozana na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Balozi Amina Salum Ali, pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed.
Mjini Amman Jordan.
Baadae Waziri wake anayehusika na Mipango na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa pia Mwenyekiti wa Mfuko wa Maendeleo wa Mfalme Abdullah Bwana Imad Fakhoury atapata wasaa wa kuwasilisha mpango wa maendeleo wa Taifa hilo.
Mpango huo umekuja kufuatia mabadiliko makubwa ya uchumi yaliyofanywa na Nchi hiyo ndani ya kipindi cha miaka kumi iliyopita pamoja na kutafuta mbinu ya kupata utulivu na Amani wa Mashariki ya Kati na Kanda ya Afrika kutokana na wimbi kubwa la wakimbizi lililosababishwa na vita kwenye maeneo hayo.
Jordan imekuwa muandaaji maarufu wa Jukwaa la Dunia la Uchumi { World Economy Forum }kwa takriban mara Tisa sasa na 16 kwa Kanda na Mashariki ya Kati ya Kaskazini mwa Afrika ambapo Viongozi wa Mataifa ya palestina, Misri, Kosovo, Iraq, Tanzania na Morocco wanatazamiwa kushiriki Jukwaa hilo.
Jukwaa la Uchumi la Dunia { World Economy Fforum - WCF} limeasisiwa Mwaka 1971 chini ya Muanzilishi na Mwenyekiti wake Profesa Klaus Schwab huko Davos, Switzerland.
No comments :
Post a Comment