Jana Mei 15, 2017 Taarifa Kutoka Ikulu zilieleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ameivunja rasmi Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu ya Mji wa Dodoma - CDA.
Baada ya Hatua hiyo Mbunge wa Kigoma mjini na kiongozi mkuu wa Chama Cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Facebook aliandika hivi..
"Kuvunjwa Kwa CDA kunapaswa kuendana na kuipanga upya Manispaa ya dodoma Kwa kuwa na Mamlaka mbili za Serikali za Mitaa Kama ilivyo sasa Nyamagana na Ilemela.
Kuvunja tu. CDA ni kutibu dalili za magonjwa na sio kutibu ugonjwa wenyewe. Rais anapaswa kuunda Jiji la Dodoma lenye kata 20 za mjini na Manispaa ya Dodoma yenye kata zilizobakia za nje ya mji kuzunguka Jiji la Dodoma. Jiji la Dodoma Ndio lirithi CDA.
Sina hakika Kama uamuzi huu sio REACTIONARY." Aliandika
No comments :
Post a Comment