Top Leaderboard Advert

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Zanzibar Diaspora

High class shops @ Fuoni

High class shops @ Fuoni

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Adsense Marquee

Monday, July 17, 2017

HII NI AIBU JAMANI!!!

Wananchi Kigoma watafuta huduma za Afya Burundi

Zahanati za vijiji vya Kagunga  na Zashe katika kata ya Kagunga halmashauri ya wilaya ya Kigoma mkoani Kigoma, hazina uwezo wa kuhudumia zaidi ya wananchi elfu ishirini na nne kutokana na kuwa na wastani wa mtumishi mmoja, ukosefu wa maabara ya vipimo na vifaa tiba muhimu hali inayolazimu baadhi ya wagonjwa kuvuka mpaka wa Tanzania na Burundi na kwenda kutibiwa katika mji wa Kabonga nchini Burundi.
Wananchi pamoja na mganga pekee aliyekutwa akitoa huduma kwa zaidi ya watu mia tano wengi wakiwa akinamama Athanas Migomba wamesema zahanati hizo mbili ambazo ziko vijiji vya mwambao wa ziwa Tanganyika na umbali wa masaa sita kwa boti kufika mjini Kigoma, vinahitaji msaada wa uboreshaji huduma za afya na hasa upasuaji.

Kwa upande wake mratibu wa shirika la kimataifa linaloshughulika na afya ya uzazi Engender heath Dr.Wilfred Mongo, amesema kutokana na changamoto zinazovikabili vijiji vya pembezoni mkoani Kigoma, shirika hilo linasaidia utoaji vifaa, ujenzi wa majengo muhimu ya hospitali na elimu kwa wataalam.

No comments :

Post a Comment