dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, November 30, 2018

PBZ yabadilisha mfumo mpya wa Kibenki!

Benki ya Watu wa Zanzibar(PBZ), imesema imepata mafanikio makubwa baada yakubadilisha mfumo mpya wa kibenki ujilikanao 'Banks' ikiwemo huduma ya kutuma fedha katika akaunti za ndani za PBZ na nje ya nchi.

Akizungumza leo na waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo,Juma Hafidhi alisema mfumo huo umeondoa changamoto zilizokuwepo ambazo zilikuwazikiwapatia usumbufu wateja na kwamba kwa sasa imeleta mafanikiomakubwa ambapo awali kabla ya mfumo huo katika ufungaji wa hesabu kwasiku ilikuwa ikichukua muda wa masaa matatu lakini kwa sasa dakika 10.Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa baada ya kubadilisha mfumo huo sasa mtu ambaye ni mteja wa PBZ kutuma pe sa kwa mtu ambae ni si mteja wa benki hiyo na kuweza kuchukua fedha yake katika tawi lolote la benki hiyo.

"Mfumo huu pia unamwezesha mtu kutuma fedha kwa mteja wa PBZ na kumpelekea mtu ambae si mteja wa benki yetu ambae ataweza kutowafedha katika ATM za benkiya PBZ,"alisema Mkurugenzi huyo Katika maelezo yake Hafidhi alitaja baadhi ya mafanikio hayo nimuajiri kulipa mishaharaya wafanyakazi wake ambao wana akaunti katika benki yeyote iliokoTanzania na nje ya nchi.

Alisema PBZ inatarajia kuanza kutumia mfumo huo mpya Desemba 3, mwaka huu na kuachana nakutumia mfumo wa zamani na kwamba kutokana na mabadiliko hayo Desembamosi mwaka huuhakutakuwa na huduma za kibenki katika matawi ya PBZ.

"Pia, Desemba mosi mwaka huu hakutakuwa na huduma za ATM na mobile Banking hazitapatikanakwa siku hiyo na kwamba huduma hizo zinatarajiwa kurejea Desemba 2 mwaka huu na hayayote yanatokana na mabadiliko haya ya mfumo huu mpya,"alisema Mkurugenzi

Mkurugenzi huyo alisema katika mafanikio hayo yanasaidia kuondoa usumbufu kwa watejakwa wanaofanya uhamisho wa fedha au kulipa cheki kutoka Islamic Banking kwenda Conventional.

Alisema PBZ inatarajia kuanzisha huduma ya PBZ mobile App  ambapo itamwezesha mteja wa benki kufanya malipo kwa wazabuni wenyeakaunti katika PBZ nabenki nyingenezo zilizoko Tanzania.

Mbali na hayo, Mkurugenzi huyo alisema PBZ inatarajia kuagiza mashine 7 za ATM ambazo zitasambazwa nje ya Zanzibar kwa lengo la kutoa huduma katika maeneo ya vijijini kwa kuwaletakaribu na wateja wa benki hiyo.

No comments :

Post a Comment