zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, December 25, 2018

IS TUNDU LISSU SLOWLY LOSING HIS MIND IN BELGIUM?

ABOVE: THE MAGNIFICENT AND AWE-INSPIRING LISSU!

Lissu tunampenda kutokana na ideas zake za kimaendeleo na ukakamavu wake (remember: 37 bullets and he is still alive), lakini kama huu ujumbe wa hapa chini kautoa yeye kweli basi Kaka Lissu itakuwa kakosea sana, tena sana. 
Hizi criticism nyengine hazina maana na wakiendelea hivi wapinzani watakuwa wanajiangusha na kujiuwa wenyewe. 
Of course sote tunajua kuwa hii ndege ni ndogo sana na huwezi kuilinganisha na models nyengine za Airbus, lakini sisi ndio kwanza tunaanza. Anataka kwa kuanzia tununue A380 tushindane na Emirates Airlines? Au kwasababu ni ndege ndogo anataka watu wasifurahi?
Akumbuke Lissu wapi tunatoka! ATC ilikuwa tayari muflis na mpaka licence ilikuwa ishaporwa. 
Mwanao anapoanza kusimama dede unafurahi na husemi ndio nini, eti kwasababu mtoto wa fulani anakuenda mabio. Na yeye atakuenda mabio, lakini kwanza lazima apitie kusimama dede.
Furaha yao sio ushamba bali ni katika kukifurahia hicho hicho kidogo chao.
Kama sisi Zanzibar hata tukipata gari la ng'ombe linaloruka basi tutafurahi, kwani hio itakuwa kwetu ni hatua nzuri in the right direction.


MWANASHERIA MSOMI ANATUAMBIA

Na. Tundu Lissu

Ushamba kitu kibaya sana. Kwenye Airbus family kuna A210, A220, A230, A310, A320, A330, A350 na, kubwa zaidi na most advanced, ni A380 Super Jumbo. 

Ukiona ina namba za ziada mbele, k.m. A220-200 maana yake ni extended range, i.e. imeongezewa masafa ya umbali wa ziada. Sasa A220-300 ni ndege ndogo sana katika Airbus family. 

Kwa sababu ya ushamba wetu, tunazungumza as if tumenunua ndege ya kisasa kuliko zote zilizowahi kutengenezwa na Airbus Industrie. 

Na hakuna anayejaribu kuilinganisha na modeli nyingine za Airbus au hata kujiuliza kwa nini inaitwa A220-200 wakati kuna nyingine zinaitwa A330, A350 au A380. 

Tunachekesha na tunachekwa na kila anayejua mambo haya lakini wala hatujielewi!!!

2 comments :

  1. kwa hapa mmesema kweli, wapinzani watafute vizuri yakulaumu na sio kila kitu

    ReplyDelete
  2. "........Kama sisi Zanzibar hata tukipata gari la ng'ombe linaloruka basi tutafurahi........"

    Sasa hilo gari litaruka na ng'ombe wake au gari tupu????
    kwi kwi kwi kwi kwi
    Nyinyi Wazanziberi ni wachepe kweli!!!!

    ReplyDelete