Balozi wa Tanzania nchini Marekani,Wilson Masilingi na Mbunge wa Sigida Mashariki
wamekutana kwenye mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya Radio America (VOA).
Katika mahojiano hayo Balozi huyo amesema kitendo cha Lissu kuzunguka dunia nzima hakisaidii. kufanya mazungumzo na BBC, Radio Ujerumani-DW, Sauti ya Amerika-VOA, sio mahakama, anachofanya ni kuchafua nchi na kutuvunjia heshima.
“Kutotambua kazi nzuri ya serikali ukazunguka dunia nzima unamtukana rais wako, vyombo vya
dola, na kuwaambia watanzania kwamba hamna haki nchini kwenu sio sawa,” amesema Balozi huyo.
Lissu alipoulizwa lengo lake la kutembea nchi za nje akieleza hali ya taifa la Tanzania na
vitendo vya mashambulizi alivyofanyiwa kuwa ni kitendo cha kulichafuwa taifa au yeye kuwa ni adui wa Tanzania, alieleza;
“Lazima tutafautishe kati ya serikali na taifa. Serikali ya Magufuli sio taifa. Serikali inatakiwa kuongozwa na katiba, na katiba yetu imeweka wazi mipaka ya mamlaka, sisi raia ambao ndio taifa tunahaki ya kuwakosoa viongozi wetu,” ameeleza.
Tundu Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, yupo katika ziara ya siku 10 nchini Marekani baada ya kufanya hivyo kwenye nchi za Ujerumani na Uingereza.

No comments :
Post a Comment