Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, February 7, 2019

JOHN HECHE AZUWA TAFRANI BUNGENI KUHUSU MJENZI WA STIEGLER SGEORGE!

MBUNGE MACHACHARI WA UPINZANI MHE JOHN HECHE.

MBUNGE wa Tarime Vijijini (CHADEMA), John Heche, amezua tafrani bungeni, kufuatia hatua yake ya kuituhumu serikali kuwa imejifunga kwenye mkataba wa kitapeli na kampuni ya J.V Arab Contractors. Anaripoti Mwandishi Wetu kutoka Dodoma … (endelea).

Akizungumza wakati akichangia taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Heche alisema, kampuni hiyo kutoka nchini Misri haina uwezo wa kufanya kazi iliyopewa na serikali.

Alisema, “kaampuni hii ya J.V Arab Contractors iliyopewa kazi ya kujenga bwawa la kuzalisha umeme kwenye Mto Rufiji maarufu kama Stieglers Gorge, haina uwezo wa kufanya kazi hiyo. Haijawahi kufanya hiyo kazi na haina uwezo wa kuifanya.”

Kwa mujibu wa Heche ambaye ni mjumbe wa kamati ya nishati, “J.V Arab Contractors, ni kampuni inayojishughulisha na kazi za ujenzi wa majumba, siyo ujenzi wa mabwawa ya umeme.”

Alisema, “hawa watu hawana uwezo wa kujenga bwawa la umeme. Kwa sababu, hiyo sio kazi yao. Kazi ya Arab Contractor ni kujenga majengo ya nyumba. Siyo kujenga mabwawa. Ndio maana baada ya kupata kazi hiyo, imetafuta mtalaamu wa kujenga hilo bwawa.”

Mara baada ya Heche kuibua madai hayo, haraka naibu waziri wa nishati na madini, Subira Mgalu alisimama na kutoa taarifa bungeni kuwa mbunge aliyekuwa anachangia (Heche), amelidanganya Bunge.

Akitumia kauni ya 64 (e) inayokataza mbunge kusema uwongo bungeni,Mgalu alisema, maelezo ya Heche kuwa kampuni hiyo haina uwezo siyon ya kweli, na kwamba yeye kama naibu waziri mwenye dhamana ya nishati anaweza kulithibitishia Bunge kuwa mbunge huyo amedanganya.

Akamtaka Heche kuthibitisha anachokisema, vinginevyo akamuomba Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson Mwansasu, kutumia madaraka yake kumuamuru mzungumzaji, kufuta madai yake.

Akijibu mwongozo wa Naibu Waziri Mgalu, Naibu Spika Tulia alisema, kwa kuwa mkataba huo uko mikononi mwa serikali na yeye hajawahi kuuona anaagiza uletwe bungeni ili kujulikane nani mkweli kati ya Heche na serikali.

Alisema, “mkataba ulifika bungeni ndipo nitakapomtaka mheshimiwa Heche kuthibitisha madai yake. Lakini kwa sasa, naamuru kusimamisha mjadala juu ya Stieglers Gorge na kwa msingi huo, mheshimiwa Heche ataendelea na mchango wake bila kuzungumzia suala hilo.”

Maamuzi hayo ya Dk. Tulia yalipokewa kwa shangwe na upande wa upinzani, huku Zitto Zuberi Kabwe, mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), akisimama katikati ya mjadala na kusema, “mimi niko tayari kumsaidia Heche kuthibitisha.”

Kauli ya Zitto, ilipingwa na baadhi ya wabunge wa CCM, wakiwamo mawaziri kwa kusema, bila kufuata taratibu, “hatutaki. Tunataka Heche mwenyewe athibitishe.”

Kampuni ya J.V Arab Contractors ilijifunga kwenye mkataba na serikali kupitia Shirika la umeme la taifa (Tanesco), ili kujenga bwawa la kuzalisha  megawati 2100 za umeme katika mto Rufiji. Mkataba kati ya pande hizo mbili, ulifungwa Ikulu ya Dar es Salaam, tarehe 12 Desemba mwaka jana.

Katika utiaji sahihi wa mkataba huo, Rais wa Jamhuri, John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu wa Misri, Mostafa Madbouly, walishudia tukio hilo lililoitwa na serikali ya Tanzania kuwa la “kihistoria.”

Wengine walioshuhudia, ni Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu; Waziri Mkuu wa Jamhuri, Kassim Majaliwa; Spika wa Bunge, Job Ndugai; Waziri wa Nishati, Medard Kalemani; Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco Dk. Tito Mwinuka na mwanasheria wa shirika hilo, Isdori Nkindi.

Wengine waliohudhuria, ni baadhi ya mawaziri, Jaji Mkuu na baadhi ya viongozi wa vyama vya Siasa, viongozi wa madhehebu ya kidini na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Kulingana na taarifa kutoka ndani ya serikali, mradi huo utagharimu kiasi cha dola za Kimarekani 2.9 billion (sawa na Sh. 6.5 trilioni).

Fedha zinazotekeleza mradi huu, ni mkopo kutoka benki moja ya kibiashara nchini Misri.

Mradi utajengwa katika hatua nne ambazo ni ujenzi wa ukuta, ujenzi wa tuta lenye uwezo wa kutunza mita za ujazo 35.2 bilioni za maji, ujenzi wa mtambo wa kuzalisha umeme wenye mashine (turbines) 9 na kujenga vituo (sub-stations) za kufua umeme wa KV 400.

Hata hivyo, mradi huo unapingwa vikali na nchi wahisani, wakiwamo hasa Ujerumani na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), kwa madai kuwa unahatarisha mazingira na viumbe asili.

No comments :

Post a Comment