Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere asidhani kama Ofisi hiyo aliyoteuliwa kama ni safi.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo Jumatatu, Novemba 4, 2019 wakati akiwaapisha wateule wake Ikulu jijini Dar es Salaam.
“Lakini pia kasimamie hii ofisi, kuna baadhi ya watendaji wako wakitumwa kukagua kwenye balozi, wanalipwa hela na bado wakifika huko wanaomba tena hela…ofisi ya CAG sio safi kama mnavyofikiria,” Rais John Magufuli.
Aidha Rais Magufuli ameongeza kuwa “Usije ukaenda huko ukajifanya na wewe ni muhimili, mihimili ni mitatu tu na umeiona hapa, nafasi yako ni Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na mwenye serikali yupo."

No comments :
Post a Comment