Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, November 4, 2019

Spika Ndugai amkaribisha CAG mpya Bungeni!

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amemkaribisha Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere na kumueleza kuwa yeye ni jicho la Taifa.
Ndugai ameyasema hayo leo  katika hafla ya kuapishwa kwa CAG iliyofanyika Ikulu, Jijini Dar es Salaam.

“Tunakutegemea sana kama jicho letu, maana jicho ndiyo kila kitu kwa mwanadamu, bila jicho huwezi kujua unaelekea wapi, kwa hiyo wewe ni chombo muhimu sana kwa Taifa. Ni jicho la Taifa,” amesema Ndugai.
 “Kazi yako ni nzito sana ila nakuahidi kwa niaba ya Bunge, tutakusaidia na kukupa ushirikiano utakaohitaji na tunaamini imani ya mheshimiwa Rais kwako utailinda na kuitunza kama kiapo chako ulichokitoa hapa leo.”

Spika huyo amemwambia kuwa taarifa yake inapowasilishwa bungeni, ni miongoni mwa taarifa muhimu, inapokelewa na wabunge na wanaichambua na kuijadili kwa umakini mkubwa.

No comments :

Post a Comment