Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, January 25, 2020

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI CANADA WAAKHIRISHA MKUTANO WA WANA-DIASPORA NA BALOZI MPYA!


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi Dkt. Mpoki Ulisubisya baada ya kumuapisha kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 20, 2019.
Barua pepe imetolewa na ubalaozi wa Tanzania nchini Canada tokea tarehe 21 January, 2020 kuwafikia Wana-Diaspora yenye kichwa cha maneno - KUAHIRISHA MKUTANO. Barua hio imeahirisha mkutano ambao ulikuwa uwe leo jijini Ottawa, Canada baina ya balozi mpya wa Tanzania nchini Canada na Wana-Diaspora wa kutoka Tanzania wanaoishi nchini Canada.

Kama inavyokumbukwa kuwa Canada kwa muda mrefu ilikuwa haina balozi baada ya aliekuwa balozi Bw. Alphayo Kidata kutumbuliwa tarehe 8 November, 2018.

Bwana Alphayo Kidata anaweza kuwa ni mtu pekee katika Serikali ya Awamu ya tano ambaye ameweza kushika nafasi zaidi ya nne muhimu katika muda mchache tangu mwaka 2015. Akitoka kuwa Katibu Mkuu wa Ardhi, Nyumba na Makaazi na kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato, baadae akawa Katibu Mkuu Ikulu na pia akawa Balozi wa Tanzania nchini Canada na sasa ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara tangu Septemba 20, 2019.

Wapili kutoka kushoto ni Bw. Alphayo Kidato akijumuika na Wana-Diaspora wa Canada katika sherehe ya kumkaribisha yeye nchini Canada tarehe 18 August, 2018 mjini Ottawa, kabla hajatumbuliwa.

Balozi mpya wa hivi sasa ni Mhe Dkt. Mpoki M. Ulisubisywa, ambae aliapishwa na Rais Magufuli katika mwezi wa May, 2019

https://zanzibarnikwetu.blogspot.com/2019/05/baada-ya-mhe-alphayo-kidata-kutumbuliwa.html


Habari ya kufika kwa balozi mpya Canada ilitolewa na ubalozi kwa Wana-Diaspora wa Canada katika mwezi wa July, 2019.


Wana-ZanzibarNiKwetu wanamtakia balozi mpya Mhe Dkt. Mpoki M. Ulisubisywa kila la kheri katika kazi yake ngumu ili iwe nyepesi.

Barua hio ya ubalozi kuena kwa Wana-Diapora inanukuliwa hapa chini kama ilivyopokelewa.

"Ndugu, Wana-Diaspora,

Ubalozi unapenda kutoa taarifa kuwa, Mkutano kati ya Ubalozi na Wana-Diaspora, uliopangwa kufanyika tarehe 25 Januari, 2020 umeahirishwa kutokana na baadhi ya Jumuiya za Wana-Diaspora kuwa na shughuli nyingine kwa siku hiyo. Hata hivyo, waliothibitisha kushiriki kwa siku hiyo wamekuwa wachache sana. Tunawashukuru Wana-Diaspora kutoka Toronto waliothibitisha ushiriki wao, Ubalozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.

Kutokana na hali hii, Ubalozi unaomba wana-Diaspora kupitia viongozi wa Jumuiya zao, wachague siku nyingine ambayo itakuwa ni muafaka kwenu, ili siku hiyo ipangwe kwenye Ratiba ya Mhe. Balozi. Mhe. Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya, anayo hamu kubwa ya kukutana Watanzania wenzake, hivyo anayo matumaini makubwa kuwa, siku ambayo itapangwa tena, wengi wenu mtashiriki. Siku ambayo itakuwa imekubalika, viongozi mnaombwa kuwahamisishe Wana-Diaspora wenzenu kuhudhuria.

Ubalozi unawtakia kila heri katika majukumu yenu.

Ubalozi – Ottawa".

No comments :

Post a Comment