BURIANI BAIT EL AJAIB MPAKA BAADAE
Kwaheri babu yetu tuliyekuwa tukikuita Jumba la Ajabu, ulieletwa duniani na Mfalme Barghash 1833 kwa nia njema kabisa.
Na ulipojengwa ulikuwa JUMBA la ajabu kwa ukubwa wako, urefu wako na haiba YAKO. Tuka kupenda.
Hata ulipopigwa mizinga wa rekodi ya vita vifupi kabisa duniani hapo na kudumu dakika 38 bado umebaki jengo kubwa.
Ulipoletwa duniani hukudhania utakuwa sio tu kipenzi chetu bali alama ya nchi yetu Zinjibari kama ulivyo Mnara wa Paris, au ule wa New York au London Bridge nchini Uingereza.
Ulitumika kama eneo la sherehe na kisha ukawa ofisi kuu ya Serikali ambapo Ukoloni uliendeshea shughuli za kiutawala humo.
Na ulipojengwa ulikuwa JUMBA la ajabu kwa ukubwa wako, urefu wako na haiba YAKO. Tuka kupenda.
Hata ulipopigwa mizinga wa rekodi ya vita vifupi kabisa duniani hapo na kudumu dakika 38 bado umebaki jengo kubwa.
Ulipoletwa duniani hukudhania utakuwa sio tu kipenzi chetu bali alama ya nchi yetu Zinjibari kama ulivyo Mnara wa Paris, au ule wa New York au London Bridge nchini Uingereza.
Ulitumika kama eneo la sherehe na kisha ukawa ofisi kuu ya Serikali ambapo Ukoloni uliendeshea shughuli za kiutawala humo.
Ukawa sehemu ya mawasiliano ambapo wasio kuwa na radio au waliopenda kubarizi kwa urojo jioni na magharibi walifungiwa mabomba kusikiliza Sauti ya Zanzibar. Enzi za miaka 50 na 60.
Ila mwenzetu ukaanza kupata shida mara tulipopindua utawala wa kikoloni ndipo ulipo anza tu sio kudharauliwa, bali kufujwa kwa kila aina. Hakuna aliyejali kukutunza... Mara kumbukumbu ya ASP, Mara Chuo cha CCM, mara sehemu ya maonyesho, mara sijui nini... Lkn ikawa kama punda wa Maruhubi kupigwa kazi bila ya maji seuze kilo za kunde au majani.
Miaka ya jumba letu kujenga mpaka tulipolitia mkononi kwa Mapinduzi na kuli fanya kitega Uchumi, yaani 1883 hadi 1964 ni 81...haikufika mengine 81 jengo limepukutika likiwa ndani ya nchi huru.
Hatukutoa umuhimu unaostahiki kwa alama zetu za Taifa... Kwamba hata kitu kama hicho kisimame kwa nguvu ya wageni.. Misaada imetuharibu.
Wageni wenyewe wenye sauti akina Shirika la Utamaduni la UNESCO tunakataa maelekezo yao juu ya utunzaji wa Mji Wa Urithi wa Dunia.
Kwa miaka mingi ijayo wageni watauliza iko wapi Beit Al Jaib... Leo baadhi wameshuhudia ikianguka kama Ukuta wa Berlin...
Pengine kitabaki kifusi tu... Pengine tutapata wahisani wa kutujengea.. Pengine kitabaki Kiwanja na sitaki kufikiria.. Nilishuhudia eneo la Twin Towers wiki mbili baada ya kuangushwa lakini alama ile ya New York ikafanyiwa kila njia pakarudi japo sio kama AWALI.
Tuliowahi kufaidi jengo hilo zaidi kwa kuwa tumekuwa na kuishi mjini ni kidogo sana... Na naamini kizazi cha chini ya miaka 25 hata hao wa mjini... Wamekuwa wakiliona jengo hilo katika hali ya masikitiko.
Kama lingeweza kusema basi lingepiga kelele kuwa tumelidharau kupita kiasi mpaka limekata roho. Chembilecho @Othman Miraji hata hitma na kula halua yake hatutafanya.
Tangu lini Wazanzibari tunajali Utamaduni wetu... Ngoma zote tulonazo Naambiwa eti kuna Ngoma hupigwa kupokelewa makampuni ya ndege yanayokuja ambapo kina mama hucheza machuchu nje... Ifike hivyo basi?
Na sisi si ndio twenye msemo kuwa asie mila ni mtumwa... Tuwe watumwa mara ngapi kuwa leo Sanaa ya Zanzibar ihaba mno madukani?
Haya Buriani babu yetu. Tulikuwa nawe na unatuondoka... Tukiwa tunakutaka bado.
Mimi ni katika wachache nitaeamini kama utarudi maana fedha zitazohitajika ni hatari... Na marafiki wamekuwa wachache sana.
Ila nitaomba urudi... Maana ile raha ya kurudi Unguja ukapata uhakika kuwa upo salama nyumbani ni kuliona jengo hilo chembilecho @RashidRabia.
Ila napata moyo uongozi wa sasa unaweza kufanya jambo. Maana moja ya lilotudhuru ni kulijumuisha jengo hilo kuwa ni alama ya chuki za ukoloni na utumwa hadi kuuliwa uongo kuwa nguzo zake wamezikwa watu.. Si hasha wapo waliolifanyia vitimbi.
Kuna dalili uongozi wa Dk Mwinyi na Maalim Seif watasafisha fikra hizo kwa faida ya #ZanzibarMoja na kwa hivyo naamini kila njia watafanya jengo lisimame tena... Japo ikiwa ni alama moja tu (the only legacy) ya utawala wao watayoiacha.
Maana Zanzibar bila ya Beit el Ajab haifikiriki
Ally Saleh Alberto
No comments :
Post a Comment