AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, December 10, 2015

Majaliwa ageukia Soko la Kariakoo

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifanya usafi katika maeneo ya Soko la Kariakoo, Dar es Salaam jana.
By Bakari Kiango, Mwananchi
Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki na viongozi wa soko la Kariakoo kukutana naye ofisini kwake Jumatatu ijayo kujadili namna ya kuliendesha soko hilo.
Majaliwa alitoa agizo hilo baada ya kushiriki kufanya usafi na wafanyabiashara wa soko hilo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli la  kufanya usafi ikiwa ni madhimisho ya  miaka 54 ya Uhuru wa Tanganyika jana.
Waziri Mkuu alifika katika soko hilo saa 1.45 asubuhi na kupokewa na Sadiki, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi na Ofisa Mtendaji wa Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (Dawasco), Cyprian Luhemeja.
Wakati akiendelea kusalimia  viongozi hao, wananchi na wafanyabiashara wa Kariakoo walianza kuongezeka wakipaza sauti na kuimba ‘jembe, jembe na wengine mafisadi imekula kwao…’
Baadhi ya wananchi waliacha kufanya usafi wakitaka kumwona kiongozi huyo akifanya usafi. Baadhi ya walisikika wakihoji, “Hivi ndiyo huyu tunayemsikia akiwafukuza watendaji wazembe TRA?”
Baada ya kusalimiana, Majaliwa alikwenda moja kwa moja katika eneo la mtaro na kuanza kufanya usafi, baadaye aliingia ndani ya jengo la soko. Hata hivyo, kazi hiyo haikuwa rahisi kutokana na umati uliofurika ukitaka kumuona,  jambo ambalo liliwapa walinzi wake wakati mgumu.
 “Nimefurahishwa na ushiriki wenu leo (jana). Nimetembelea soko hili hadi kule shimoni, hata hivyo mazingira ya soko hili bado yanahitaji uboreshaji mkubwa.
“Nataka viongozi wenu wa soko wakishirikiana na Sadiki waje ofisini kwangu Jumatatu, wanieleze na kunishawishi mpango mkakati wao wa kuliendesha soko hili,” alisema  Majaliwa baada ya kumaliza kufanya usafi huku akishangiliwa na umati huo.
Aliwataka Watanzania kufanya kazi ya usafi kuwa endelevu kwa kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha nchi inakuwa safi na kivutio kwa wageni wanaokuja kuitembelea, ambao anaamini watakuwa mabalozi wazuri pindi watakaporudi katika nchi walizotoka.
“Rais John Magufuli ameanzisha kaulimbiu ya ‘Hapa ni Kazi Tu’, sasa nataka iwe endelevu na kuwa ‘sasa ni kazi tu’. Tuiendeleze na kila Mtanzania akiamka ajue ni kazi tu,” alisema Majaliwa.
Pia, aliwataka Watanzania kuondoa  wasiwasi juu ya operesheni ya kuwatafuta wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi bali waendelea kufanya biashara zao kama kawaida, lakini ziwe halali na wakumbuke kulipa kodi.
Alisema Serikali yake imepanga kukutana na wakuu wa mikoa na wakurugenzi, ili kujadili namna ya kuwawezesha wafanyabiashara wadogo kwa kuwatengea maeneo maalumu ya kufanya biashara zao bila bhughuza.
“Tunataka kufanya maboresho makubwa kwa wafanyabiashara, pia tunataka kuachana na habari ya kufukuza fukuza vijana wetu. Chini ya Dk Magufuli  tunataka kila mtu afanye biashara au kazi kwa amani na utulivu,” alisema Majaliwa.
Aliwaahidi wafanyabiashara  kuwa atapanga siku maalumu ya kutembelea soko la Kariakoo ili kusikiliza matatizo na kero zinazowakabili.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco, Mhandisi Luhemeja alisema taasisi yake imejipanga kutoa huduma nzuri ili kuhakikisha Watanzania wanapata maji safi na salama.
Pia, alisema Dawasco imejipanga kutoa elimu kwa wananchi namna bora ya kutunza chemba za maji ili kuondoa kero na malalamiko kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam baada ya chemba hizo kupasuka na kutiririsha maji hovyo.

No comments :

Post a Comment