Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, February 16, 2016

Vigogo wanne wang’olewa Bodi ya Mikopo


Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako. Picha ya Maktaba
By Beatrice Kabojoka, Mwananchi Digital
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako amemfuta kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), George Nyatenga kwa utendaji usioridhisha.
Wengine waliositishiwa mikataba ni pamoja na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Yusufu Kisare, Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo Juma Chagonja na Mkurugenzi wa Upangaji na Utoaji Mikopo Onesmo Laizer.
“Nasitisha mkataba wake (Nyatenga) mara moja na hmna haja ya kumwandikia notisi, apewe mshahara wa mwezi mmoja,” amesema Profesa Ndalichako.
Pamoja na usitishaji wa ajira za wakurugenzi hao, Waziri Ndalichako ameagiza  kufanyika ukaguzi wa ndani kwa lengo la kuhakiki nyaraka zilizowasilishwa Bodi ya Mikopo pamoja na kufanya ukaguzi maalum kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2013 hadi sasa.

No comments :

Post a Comment