Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, August 27, 2012

CCM YASAMBARATIKA NYUMBANI, LAKINI YAIMARIKA WASHINGTON DC!

Na  Geo Kimbi wa Wagagagigikoko.

Wakati Chadema yavuna wanachama zaidi ya 3,500 wakiwemo viongozi wa CCM katika operesheni maalumu ya Chama hicho ya ‘Vua gamba vaa Gwanda’ inayoongozwa na Chama hicho huko Tarime mkoani Mara, CCM yang'ara huko Washington DC kama picha za hapa chini zinavyoonesha.
Jitihada za usiku kucha za kumpata yule muandishi machachari Abdalah Hamis (ambae sote tunategemea kuwa Ijumaa ijayo tarehe 31 Agosti kwenye gazeti la The Citizen atatoa amri kwa Tanzania kuanza mara moja kuichapa Malawi baada ya mazungumzo kumalizika vibaya, kwani kwa sasa SABABU tunayo, NIA tunayo na UWEZO tunao) ili atujulishe nini kilitokea huko Washington DC wakati Bw. Kinana alivyofungua rasmi tawi jipya la CCM DMV haikuleta faida.
Habari ambazo sizo za kuaminika zilizowafikia Wagagagigikoo hivi karibuni zinasema kuwa Toronto (Canada) nayo huenda karibuni ikafungua tawi la CCM. Kwavile Toronto haipo mbali na Washington DC tutamuomba Ndugu Abdalah Hamis afike Toronto kutafuta ukweli juu ya ufunguzi wa hili tawi jipya la CCM kaskazini mwa America.
/Kimbi

N.B.
Kaka Abdalah Hamis, nikizitizama hizi picha za ufunguzi wa hilo tawi hapa 
chini, naona bora nikuombe unichukulie na mimi kadi ya CCM ya huko DMV.
Kama haitowezekana basi bora nihamie DMV kabisa!


Mhe. Abdulrahman Kinana afungua rasmi Tawi la CCM DMV
Abdulrahman Kinana ni kanali mstafu wa jeshi, mjumbe wa taifa kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi, Spika wazamani wa Bunge la Afrika mashariki na Meneja wa Kampeni ya Mhe Rais Jk mwaka 2010.

Mgeni rasmi katika ufunguzi wa tawi la CCM DMV Mh.Abdurhaman Omar Kinana akiwa na wakekereketwa wa chama Dc.

Ufunguzi huo ulihudhuriwa na baadhi ya wapenzi wa Chama cha Mapinduzi CCM, waishio hapa DMV  Siku ya Jumamosi Aug 25, 2012 katika ukumbi wa Martin Luther King Jr Hwy Lanham, Maryland. Nchini Marekani.
Mh.Abdurahman Kinana kutoka kushoto Anti Grace Mgaza Sebo, Eda na kulia kwa Mheshimiwa Zay B na Fatuma Mwamba a.k.a Miss Kigoma.

Mh. Loveness Mamuya kipenzi cha umma akipata flash ya pamoja na Wash kutoka All the way from Cleveland Ohio.

 Mh. Loveness Mamuya akiwa pamoja na mwanachama wa CCM DMV.

Ma Winny Casey Khanga Wrap Designer akipata flash ya pamoja na Mercy Mfanga-Ligate katika ufunguzi rasmi wa Tawi la Chama cha Mapinduzi DMV.

Mwenyekiti wa Tawi la CCM DMV Loveness Mamuya akipata flash ya pamoja na mdhamini wa pendo la Rubani  Bw.Stephano Mhina, na salam ziwafikie popote pale ulipo jiji Dar es salaam.

Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wakipata picha ya pamoja na mwenyekiti wa Tawi hilo

Ninani asieee mjuaa Halima Ali kama ni mwana ni Mzaliwa wa Chama cha Mapinduzi CCM. (Vua Gwanda Chana Gamba vaa Uzalendo)

Mwanachama hai wa CCM Dedie Rouba akipata flash na Hafsa Bin Khami Bin London katika ukumbi wa Martin Luther King Jr Hwy Lanham, Maryland. Nchini Marekani.

(Vua Gwanda Chana Gamba vaa Uzalendo) Mwenyekiti wa Tawi la CCM DMV Loveness Mamuya akiwa na wanachama wa CCM, na bendera ya chama hicho jana Jumamosi katika ufunguzi wa tawi hilo.

Katibu Yacob Kinyemi  akiwa na Msalem

Picha ya Mwenyekiti imebidi tuitoe mara mbili, kwasababu uenyekiti sio kazi ndogo hasa kikiwa chama chenyewe ni cha CCM. Bw. Abdalah Hamis ukishindwa kunipatia kadi, basi nitaikata kadi mwenyewe moja kwa moja kutoka kwa Mwenyekiti, japokuwa najua kuwa hii sio njia ya kupita kwa mwanachama mpya kama mimi. Malipo na ada ya kila mwezi yatakuwa kwa pesa za madafu!

Source: Swahilivilla

No comments :

Post a Comment