dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, August 19, 2012

Jengo jipya uwanja wa ndege kuhudumia abiria 800

Na Husna Mohammed


ZANZIBAR | Abeid  Amani Karume International Airport Terminal II Extension

JENGO jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar, Abeid Amani Karume, linatarajiwa kuchukua abiria 800 wa kuingia na kutoka mara baada ya kukamilika kwake.

Meneja wa Ufundi wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Zanzibar, Mzee Abdalla Mzee, aliyasema hayo jana wakati akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari vilivyofika katika kiwanja cha kimataifa cha ndege Zanzibar, kwa ajili ya kupata maelezo juu ya ujenzi wa kiwanja hicho.


Hata hivyo, Meneja huyo alisema kuwa mara baada ya kukamilika kwake wataangalia uwezekano wa kuona kiwanja hicho kutumika kwa wageni pekee au mchanganyiko.

“Tutaangalia uwezekano kama tutumie kwa wageni pekee na wenyeji watumie ule wa awali au la”, alisema.

Aidha alisema kwa mwaka wanakusudia kuchukua abiria milioni 1.1 kwa mwaka kutoka nchi mbalimbali duniani.

Meneja huyo alisema jengo hilo litakuwa la kisasa ambalo litakuwa na ubora kama viwanja vyengine duniani.

Jengo hilo jipya la abiria limeanza ujenzi wake mwaka 2010 na kukamilika mwaka 2013, ambapo litagharimu dola milioni 70.4 ambazo ni mkopo kutoka Benki ya EXIM.

Ujenzi huo unajengwa na Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group ya China.

Chanzo: Mzalendo.net

2 comments :

  1. Ni abiria 800 kwa siku au kwa mwezi au vipi?
    Mwenyekujua atujuvye!

    ReplyDelete
  2. Naona huyu ndugu yetu kutoka Mzalendo.net kaelezea vizuri:

    "sweethome 20/08/2012 kwa 9:32 mu · Ingia kujibu
    jamani punguzeni jazba kidogo mimi nilivyofahamu ni kama hivi:
    jenge jipya linauwezo wa kuchukua abiria 800 kwa wakati mmoja, tukumbuke kwamba watu hawakai airport siku nzima.
    ukuchukua makdirio yao ya watu 1,100000 kwa mwaka. ukigawa na siku 360 za mwaka (makadirio)
    utapata kiasi cha watu 4000 kwa siku, logically hii inakubalika, ni karibu na watu 150 kwa saa.
    sasa ukilinganisha na kimoja kati ya viwanja vikubwa kabisa dunia let take cph(copenhagen ) airport, inachukua abia million 22 kwa mwaka. ukigawa na siku 360..kwa wastani wanaingia watu 60,000 kwa siku, na ni wastani wa watu 2500 kwa saa.
    ukitizama hizo tal, utaona kwamba, kwa ukubwa wa znz na population yake.kiwanja kitakidhi haja bila ya wasi wasi wowote.
    na kuhusu matumizi ya jengo, hapa kuna tricky kidogo. tufahamu kwamba viwanja vingi vikubwa duniani vimegawika sehemu mbili au tatu kwa europe, sehemu ya international, ya euro na ya local passangers. kwa kurahisisha process na kufanya uwanja uwe effectiv.
    lakini matumaini yangu hiyo sehemu itakayo tumiwa na ndege za local i we na hadhi nzuri,
    nawasilisha"

    ReplyDelete