“Karibu Zanzibar nchi isiyokuwa na Rushwa”
Zanzibar ni nchi ya ajabu sana. Ina historia nyingi pekee kama nchi ya kwanza Afrika kuwa na Televisheni ya rangi. Zanzibar ni nchi pekee Afrika yenye historia ya kimaajabu kwa kutokuwa na mdudu mbaya anayeitwa Rushwa.
Kuna Rais mmoja mstaafu aliwahi kunukuliwa akisema kwamba Zanzibar hakuna rushwa ndiyo maana hatuna haja ya kuwepo chombo kama Takukuru.
Hili ni mojawapo katika maajabu ya Zanzibar kuwa ni nchi pekee duniani ambayo haina rushwa.
Kwa nini hakuna Rushwa?
Kwasababu hakuna hata mtu mmoja aliyewahi kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kosa la rushwa.
Kwa sababu hata akifikishwa mahakamani hakuna hiyo sheria ya rushwa ambayo itaweza kumshitaki na hatimaye mtuhumiwa kutiwa hatiani.
Kwa sababu Baraza letu la kutunga Sheria ( Baraza la Wawakilishi) limeipiga danadana sheria ya Rushwa miaka dahari na kila ikiletwa Barazani hurudishwa kwa watunga Sheria waifanyie ukarabati iwe “imara” zaidi.
Kwasababu ukitajirika haraka haraka Zanzibar hakuna atakaehoji utajiri wako bali wako wengi watakaosifu ujanja nausmati wako.
Kwa sababu hatusikii viongozi wakuu wa serikali, masheikh, mapadri kuikemea rushwa kwa nguvu zote kwakuwa haipo.
Kwasababu anayekula rushwa huwa hana huruma na wenzao anajijali yeye mwenyewe tu na Wazanzibari ni watu wenye huruma sana na wenzao.
Kwasababu wazanzibari wengi ni waislamu ambao hufuata misingi ya dini yao inayowakataza kujiingiza katika vitendo vya rushwa.
Ntashindwa kuendelea ila bora nianze kujipanga nikaanze maisha yangu katika visiwa vya Zanzibar ambavyo ni vya kimaajabu katika dunia yetu ya leo.
Ningelipendekeza katika kuenzi maajabu haya, Uwanja wa ndege na bandarini liwekwe Bango kubwa linalosema “Karibu Zanzibar nchi isiyokuwa na Rushwa”
Chanzo: Mapara
Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Pita kila siku kwa habari moto moto. (This blog is about Tanzania and the world as a whole. Pass-by everyday for breaking news). ***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************
No comments :
Post a Comment