zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, September 8, 2013

ZANCANA INAVYOWAKWAMUA WANANCHI ZANZIBAR

Source: Vijimambo
                           
 ZANCANA Jumuiya ya Wazanzibari waishio Canada katika
mwezi wa August 2013 wametoa misaada mbalimbali ikiwemo
kufutarisha katika mwezi wa ramadhan, msaada wa nguo, mabegi ya 
shule kwa wanafunzi wa Mwambeladu , uniform kwa wanafunzi wa 
Rahaleo, Vitabu wa dua, Tasbeh na vito vya thamani kwa madrasa 
na nguo za madaktari na wauguzi kwa Wizara ya Afya Zanzibar.
ZANCANA tunafahamu mahitaji haya hayakidhi mahitaji ya wengi,
Wananchi wanaohitaji msaada bado ni wengi na Jumuiya hii haiwezi 
kufanya peke yake bila msaada wako kwa hiyo basi tunajua unajali na 
una upendo wa Wananchi wako sisi tumeanza kidogo tulichonacho, 
ukiangalia picha hizi utaona hawa Wananchi 
wachache walivyokua na nyuso za furaha kupata msaada huu mdogo 
kutoka ZANCANA.
Kama wewe umetokea Zanzibar au kwa yeyote yule anayependa
kusaidia Jumuiya hii anakaribishwa, vitu tunavyokusanya ni viatu 
kwa wanafunzi, mabegi ya shule na vitu vingine vinavyoweza 
tumiwa na Mwanachi na kuwezesha kusukuma maisha yake ya 
kila siku kwenda mbele. 
Tafadhali wasiliana na ZANCANA Manager Bishara Al Masroori 647 866 4312

 Picha juu na chini ZANCANA ikifutarisha.


 ZANCANA ikitoa msaada wa nguo za madaktari na wauguzi wa 
Wizara ya afya Zanzaibar.

 Juu na chini ni ZANCANA ikitoa vitabu kwa madrasa



 Picha juu na chini ni ZANCANA ikitoa misaada ya Uniform na 
magegi ya shule za Mwembeladu na Raha leo







                          

Chanzo: Vijimambo

No comments :

Post a Comment