Makongoro - The ony saviour of Tanganyika from "wizi, rushwa, tamaa, ujangiri wa rasilimali ya nchi hii na ufichaji wa pesa za kigeni huko Uswiss”!
``Kumchaguwa tena mtu alietemwa ni sawa na kula matapishi. Sidhani kama Watanzania wapo tayari kula matapishi yao``.
Baada ya mbunge wa Monduli Mheshimiwa Edward Lowassa kutamka hadharani kuwa sasa
“ameshawishika” na kuweka bayana kuwa atachukua fomu ya kugombea urais kwa
tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Blog
la Zanzibar Ni Kwetu lilitabiri hapo hapo kuwa atashinda
katika uchaguzi wa October na atakuwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya Rais Kikwete kuachia
ngazi.
Tokea
tufanye utabiri huo, tumekuwa tukijuta, kwani simu zetu hazijasimama kulia
mpaka hii leo na lines nyengine za ofisini kwetu imebidi ziwe dis-abled
temporarily, kutokana na vilio vya Wazanzibari waliokerwa na utabiri wetu huo.
Wengi katika
hao wanaotupigia simu wanatamka waziwazi kuwa wataweza kumuunga mkono kwa
mikono yote miwili Makongoro Nyerere kama atachaguliwa na CCM kugombea urais,
lakini hawatokuwa tayari kumuunga mkono mgombea mwengine yoyote yule kutoka
Bara kama Makongoro atakataa kugombea katika mwaka huu wa 2015, kwasababu
safari hii ni zamu yao Wazanzibari kuiongoza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wakijulishwa
na Blog hili kuwa hakuna kipengele chochote katika Katiba ya Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kinachoelezea kuwa urais wa nchi utakuwa wa kupokezana baina
ya Bara na Visiwani, Wazanzibari hao waliojaa hamasa walieleza kuwa…“Lazima tuuseme
ukweli. Huu ni Muungano wa nchi mbili ambazo zilikuwa huru na zilikuwa na bendera
zao wenyewe kwenye Umoja wa Mataifa. Haiwezekani Rais awe anatoka upande mmoja tu, kama
vile upande mwengine hauna watu wanaofaa. Zaidi, hao wa upande wapili mara
nyingi wanaongoza katika wizi, rushwa, tamaa, ujangiri wa rasilimali ya nchi hii na ufichaji
wa pesa za kigeni huko Uswiss”.
Alivyoulizwa
kwenye simu mmoja wao kuwa kama wanao
msimamo huo sasa kwanini wasipendekeze hivyo katika Katiba mpya? Alijibu kwa
hamaki huku akiigongagonga simu yake na kuifanya isisikike vizuri kuwa…” Hivyo
ndivyo tulivyopendekeza, lakini maoni
yetu yalitupiliwa mbali”.
Mara
mwananchi mwengine aliekuwa kwenye simu nyengine akaendelea kujibu hata bila ya
kuulizwa yeye suala hilo. ”Mlisikia na mliona wenyewe yaliomkuta mzee wetu. Mzee
wa watu katia ombi letu la serikali 3 kwenye Rasimu na bahashishi yake ilikuwa
kupigwa kiti cha kichwa. Je, kama angelitia
kwenye Rasimu kuwa wananchi wanataka urais uwe wakupokezana hivyo angeliishi
mpaka leo?”, akamalizia mwananchi huyo na simu akaikata hapo hapo kwa hamaki.
Blog hili
liliwauliza wapiga simu wengine, kwanini watamuunga mkono Makongoro Nyerere na
hawatofanya hivyo kwa mwengine yoyote yule kutoka Bara, wakati Makongoro nae
anatoka Bara pia?
”Huwezi
kumlinganisha Makongoro na hao wengine wanaolilia kuiongoza nchi hii. Wote hao ni
watumikia tumbo tu na hakuna msafi hata mmoja. Hao wengine wote washakuwa viongozi
huko nyuma na wengine ni viongozi mpaka sasa, la kujiuliza ni kuwa wamefanya
nini jema kwa nchi hii zaidi ya ufisadi nazi na wizi tu?. Zaidi, wengine Nyerere alikwisha sema kuwa hawafai, kwani
wanasifa ya kujilimbikizia mimali tu”, alimalizia kwenye simu mwananchi huyo.
“Tutamuunga
mkono Makongoro kwasababu ni mtoto wa mfanyakazi na mkulima na sio bepari. Tunajua
akipata yeye urais basi itakuwa tumeupata sisi sote wanyonge wa nchi hii. Ule ujinga na upuuzi wa mtu kukamatwa na Dollar
zaidi ya milioni moja na baadae kueleza kuwa hizo ni vijisenti tu, au mtu kutoa
milioni 10 za wizi kutoka benki na baadae kusema kuwa hizo ni pesa za mboga tu,
au watu kuhongana bilioni 330 wakati watoto wetu bado wanakaa chini mashuleni
bila ya madawati - ujinga na upuuzi kama huo utakuwa umekwisha hapa nchini chini
ya Makongoro”.
“Wewe
tayari unao ng’ombe 1,000 kwenye zizi lako, sasa kwanini hujishughulishi na
kuchunga hao ng’ombe wako na unataka kutuchunga sisi?”, aliuliza mwananchi mwengine
kwenye simu.
“With 1000
heads of cattle, unknown number of buildings for rent and hotels, you are a bourgeois capitalist, too rich to
lead this nation of poor peasants and workers. Bepari kama wewe huwezi
kutuongoza sisi walalahoi - wakwezi na wakulima. We need someone with a proven
anti-rushwa record na sio mtu alietemwa na awamu moja na sasa agombee urais
awamu nyengine. Kumchaguwa tena mtu alietemwa ni sawa na kula matapishi.
Sidhani kama Watanzania wapo tayari kula matapishi yao”, aliendelea mwananchi
huyo huku akichanganya ung’weng’we na kiswahili, kama vile kashuka leo kutoka
UK.
Ukiachilia
mbali vilio vya Wazanzibari, ishara zote zinaonesha kuwa Lowassa ndie atakae
kuwa chaguo la CCM na ndie atakae kuwa Rais wa Jamhuri. Kama ni hivyo
tunadhania kuwa atakuwa Rais wa mwanzo wa Jamhuri ambae atachaguliwa kutoka
upande mmoja tu wa Muungano. Definitely, that would not make sense to any
sensible person – even to Lowassa himself. Lakini, kama wanavyoeleza
walimwengu, mwenye nguvu mpishe. Bwana Lowassa tutampisha Ikulu, lakini bila ya
kura zetu!
No comments :
Post a Comment