Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Madaktari wa Cuba wanaomaliza muda wao wa utumishi hapa Zanzibar ambao aliwaandali chakula cha Jioni nyumbani kwake Mazizini nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Balozi Seif akisalimiana na Mkuu wa Mafunzo wa Madaktari Wazalendo wa Zanzibar waliopata taaluma chini ya Madaktari Mabingwa wa Cuba Dr. Daisy Batlle kabla ya chakula cha jioni alichowaandalia Madaktari mabingwa wa Cuba.
BaloziSeif akibadilishana mawazo na Kiongozi wa Madaktari wa Cuba Profesa Ulpiano hapo nyumbani kwake Mazizini nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Kiongozi wa Madaktari Mabingwa wa Cuba Profesa Ulpiano wa kwaza kutoka kulia akiwa pamoja na Mwenyeji wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakipata mlo kwenye hafla fupi waliyoandaliwa Madaktari hao.
Baadhi ya Madaktari Mabingwa wa Cuba wanaomaliza muda wao wa kazi hapa Zanzibar wakipata mlo wa jioni nyumbani kwake Balozi Seif Ali Iddi hapo Mazizini.
Balozi Seif akimzawadia Kasha Kiongozi wa Madaktari wa Cuba Profesa Ulpiano mara baada yam lo wa jioni kama ishara ya kumbukumbu ya uwepo wao hapa Zanzibar.
Mkuu wa Mafunzo wa Madaktari Wazalendo wa Zanzibar waliopata Taaluma chini ya Madaktari Mabingwa wa Cuba Dr. Daisy Batlle akipokea zawadi kutoka kwa Balozi Seif.
Balozi Seif Ali Iddi kati kati ya waliokaa kwenye viti akiwa katika picha ya pamoja na Madaktari Mabingwa wa Cuba wanaomaliza muda wao wa kutoa huduma za Afya hapa Zanzibar.
Picha na – OMPR – ZNZ








No comments :
Post a Comment