zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, July 17, 2015

ZACADIA FOUNDATION YA CANADA YAFUTARISHA UNGUJA NA PEMBA!

Mayatima na wanafunzi wengine wakifutari

Mtoto yatima akipokea eid yake. Angalia hio nyumba anayolala. 
Kwa kweli watoto wanastahiki kusaidiwa. Tembelea website ya Zacadia ili usaidie.
Ile Foundation ya kizanzibari yenye nia ya kusaidia kupunguza umaskini katika visiwa vya Zanzibar iliyoasisiwa mjini Toronto, Canada na ambayo kwa umaarufu inajulikana kama ZACADIA, yaani ZANZIBAR-CANADIAN DIASPORA ASSOCIATION, hivi majuzi ilifutarisha katika kisiwa cha Unguja na Pemba. 

Pia, iligawa tende kwa waumini wa kiislamu wa misikiti mbali mbali pamoja na Madrasa za akina mama. 

Zacadia pia iliwapatia eid yao mayatima wanaowadhamini Pemba na Unguja na wale wanaosoma katika shule mbali mbali nchini Tanzania na India.

Manager wa shuguli za Zacadia katika kisiwa cha Pemba Dr Said Mohammed na wa Unguja Bi Firdaus Rashid walilielezea blog la Zanzibar Ni Kwetu kuwa shughuli hizo zilikuenda vizuri kama walivyotarajia. 

Zacadia inawadhamini watoto mayatima kadhaa Unguja na Pemba kwa kuwasaidia katika maisha yao, lakini bado wapo mayatima tele wanaoonyeshwa kwenye website ya Zacadia ambao bado hawajapata wadhamini. 

Yoyote mwenye moyo wa kujitolea anaweza kupata muongozo na maelezo zaidi juu ya namna ya kumdhamini mtoto yatima kwa kubonyeza hapa:


Ahitajiki mtu awe millionaire ili aweze kumdhamini mtoto yatima, kwani ni Dollar moja tu kwa siku. Kama Dollar moja ni ngumu basi marafiki 2 wanaweza kwa pamoja wakamdhamini mtoto mmoja kwa kila mmoja kuchangia nusu Dollar (50 CENTS) kwa siku.















 








No comments :

Post a Comment