Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, August 20, 2015

Mbunge CCM Lindi ahamia CUF

Wafuasi wa CUF wakiwa katika moja ya mikutano
Lindi. Mbunge wa Viti Maalumu CCM Mkoa wa Lindi, Riziki Rurida amekihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Wananchi (CUF).
Rurida alikabidhiwa kadi ya CUF na Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika Mchinga, Lindi Vijijini.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, ilisema katika mkutano huo wanachama 650 wa CCM walitangaza kukihama chama hicho na kujiunga na CUF.
Mbunge huyo ambaye ametumikia wadhifa huo kwa vipindi viwili, alisema anajisikia mwenye furaha baada ya kukabidhiwa kadi na kuwa mwanachama wa CUF.
Rurida alikuwa ni miongoni mwa wanachama wa CCM waliowania nafasi ya ubunge katika Jimbo la Mchinga na kuangushwa na mbunge wa sasa, Said Mtanda akiwa wa pili na kulalamika kuwa uchaguzi huo ulitawaliwa na mizengwe.
Akimkaribisha CUF, Maalim Seif alisema wimbi la mabadiliko nchini linaloongozwa na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ni kubwa hakuna atakayeweza kulizuia.
“Hili wimbi ni kubwa, mnasikia vigogo wa CCM wanaendelea kuporomoka na kujiunga na wapinzani, atakayejaribu kupingana na wimbi hili atapasuka kifua,” alisema Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Maalim Seif alikemea tabia ya baadhi ya viongozi na askari polisi kuwazuia wananchi wasitumie haki yao ya kidemokrasia ikiwamo kufanya maandamano na kuwahimiza wafuate sheria na wajiepushe na uvunjifu wa haki za binadamu.
“Polisi nchini kote fuateni sheria, hamtakiwi kuingia kwenye siasa, lakini kama kuna kiongozi wa jeshi anajiona ni CCM kuliko hao CCM wenyewe, basi avue magwanda aje tupambane kwenye majukwaa ya siasa,” alisema.
Mbunge wa Lindi Mjini, Salum Barwan alisema wananchi wa mikoa ya Kusini wana kila sababu ya kuikimbia CCM kutokana na sera zake mbovu ambazo hazijawasaidia wala kuwapa matumaini yoyote.
Mtatiro achukua fomu Segerea
Wakati hayo yakiendelea, aliyekuwa naibu katibu mkuu wa CUF, Julius Mtatiro amepitishwa na Ukawa kuwania ubunge katika Jimbo la Segerea.
Katika tamko lake kupitia Facebook ambalo pia alikiri kuhusika nalo, Mtatiro alisema: “Leo chama changu kimenipa ridhaa na barua rasmi ili nigombee ubunge kwa tiketi ya Ukawa, nimetoka kuchukua fomu ya kugombea ubunge wa Jimbo la Segerea.
“Natumaini kuwa tutaanza kwa nguvu na kumaliza kwa ushindi. Nawaahidi kuwa nitaunganisha vyama vya CUF, Chadema, NCCR na NLD kushirikiana na wananchi wa Segerea kupata madiwani wa kata zote 13.”
/Mwananchi.

No comments :

Post a Comment