Madiwani 18 wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, jana walitangaza kuhama rasmi.
Madiwani hao waliwakilishwa ofisi za Chadema Mkoa wa Arusha jana na aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Elias Ngorisa aliyeambatana na Diwani wa Kata ya Engusero Sambu, Kagil Mashati Ngukwo, ambaye pia alikuwa Katibu wa Fedha na Uchumi wa CCM Wilaya ya Ngorongoro.
Pamoja nao walikuwepo wazee wa mila wa Kabila la Wamasai (malaigwanani) Laurence Ngorisa na Lekakui Oleiti, wote kutoka Engusero Sambu.
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, ndiye aliyewapokea makada hao na kuwapatia kadi za Chadema.
Akizungumza baada ya kupokea kadi, Elias Ngorisa, alisema wapo madiwani 18 kati ya 28 ambao tayari wamechukua kadi za Chadema.
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake (UWT), Wilaya ya Siha, mkoani Kilimanjaro, Susan Natai na madiwani wengine wawili, wamejitoa CCM na kujiunga Chadema.
Mbali na Natai, wengine waliojiunga na Chadema ni Denengwa Leole ambaye ni Diwani wa Viti Maalum Kata ya Kashashi, Diwani wa Viti Maalum, Tarafa ya Siha Magharibi, Eliaika Kileo na aliyekuwa mgombea wa kiti cha udiwani, Kata ya Gararagua, John Sambua maarufu kama Mwarabu.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment