Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, August 6, 2015

Wana-CCM kata ya Manzese watishia kupigia kura upinzani.

  Naomba vikao vya maamuzi vya Chama kuangalia kwa makini na kurudisha jina la mwanachama anayekubalika ili kata ya Manzese isichukiliwe na upinzani.

Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Manzese jijini Dar es Salaam, wametishia kukihujumu chama hicho kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu wakimtuhumu katibu wao kuwa amevuruga kura za maoni ya kumpata mgombea udiwani wa kata hiyo.
 
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wanachama hao walidai kuwa katibu huyo, Ramadhan Kidogo, alikuwa na mgombea wake aliyetangazwa mshindi wa kura hizo kwa njama.
 
Mmoja wa wanachama hao, Bilal Ismail, alidai kuwa katika tawi lake la Mwembeni, katibu huyo aliamuru wanachama wapige kura bila kutumia kitabu cha orodha ya wanachama (leja).
 
Mwanachama huyo ambaye aliyejitambulisha kuwa ni mjumbe wa halmashauri kuu ya tawi hilo, alisema iwapo ngazi za maamuzi zitarejesha jina la aliyepitishwa, basi wao wako tayari kupigia kura mgombea wa upinzani.
 
"Ni bora sasa tukose wote kuliko kuachia hali hii, tulitegemea kuwa kiongozi huyo angesimamia taratibu za Chama lakini alikuwa ana nia yake," alisisitiza.Kwa upande wake, Mjumbe wa Shina Namba 21 tawi la Mnazi Mmoja, Farida Abdallah, alimtuhumu katibu huyo kwamba alichangia kumpa ushindi mgombea ambaye hakutakiwa.
 
"Naomba vikao vya maamuzi vya Chama kuangalia kwa makini na kurudisha jina la mwanachama anayekubalika ili kata ya Manzese isichukiliwe na upinzani," alisema.
 
Akijibu madai hayo, Katibu huyo alijibu kwa kifupi kuwa ni uzushi na kwamba hayo ni malalamiko ya watu walioshindwa kwenye kura za maoni.
 
"Siwezi kuvuruga kura ila katika ushindani, wale wanaoshindwa huwa wana kawaida ya kulalamika na ndivyo ilivyotokea hata katika kura zetu," alisema Kidoga.
 
Naye mgombea aliyeibuka kidedea katika kura hizo za maoni, Abdulkarim Atiki, alikana tuhuma za kubebwa na Katibu huyo na kueleza kuwa madai hayo hayana ukweli wowote na kuwataka wana-CCM kutowasikiliza wanachama wanaoeneza taarifa hizo.
 
Katika uchaguzi huo, Atiki aliibuka kidedea kwa kujizolea kura 1,199 na kufuatiwa na diwani wa zamani Eliam Manumbu, aliyepata kura 1,020, Muhidin Kassim (420) na Boniface Shauritanga (207). 

CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment