Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, December 13, 2015

Ahadi za JK zazidi kukwama

Image result for kikwete

Ununuzi wa meli nne ilikuwa moja ya ahadi za Rais mstaafu Jakaya Kikwete mwaka 2010 lakini hadi anamaliza muda ilikuwa haijatekelezwa.
CCM ilichukua ahadi hiyo na kuiweka katika ilani yake ya Uchaguzi Mkuu uliopita, hata hivyo.

Wakati akitoa ahadi hiyo kwenye kampeni zake mwaka 2010, Kikwete alisema serikali ingenunua meli nne mpya na kutoa huduma ya usafiri katika maziwa hayo.

Uchunguzi uliofanywa na Nipashe hivi karibuni umeonyesha mpango wa kununua meli hizo hauwezi kutekelezeka kwa sababu ya uhaba wa fedha.

Mradi huo ambao unatekelezwa kwa pamoja kati ya Tanzania na Denmark kupitia Shirika lake la Maendeleo la Danida, ulitarajiwa kugharimu Dola za Marekani zaidi ya Milioni 80 (sawa na Sh. bilioni 160) na ulipangwa kuanza mwaka jana na kumalizika 2018.

Hata hivyo, mradi huo umeonekana kukwama baada ya serikali ya awamu ya nne kushindwa kuchangia. Chanzo kimoja kilisema serikali ya Rais John Magufuli inaweza kufufua matumaini ya nchi kupata meli mpya zitakazotoa huduma katika maziwa na baharini.

“Ni muhimu kupata meli mpya kwani zitakuza uchumi kwa kuunganisha na nchi jirani, na kurahisisha usafiri kwa wananchi ambao kwa sasa ni tatizo kwao kutoka eneo moja hadi lingine kutokana na ubovu wa vyombo vyetu,” kilisema chanzo hicho.

MELI ZILIZOAHIDIWA
Taarifa zinaeleza katika makubaliano kati ya serikali na Danida, meli zilizotakiwa kununuliwa zilikuwa mbili kwa Ziwa Tanganyika na nyingine mbili kwa maziwa ya Nyasa na Victoria.

Aidha, kwenye utaratibu huo meli nyingine tatu za Mv Serengeti, Mv Victoria na Mv Umoja inayobeba mizigo zingekarabatiwa.

Mpaka sasa meli 14 ndizo zinafanya kazi, lakini zenye uhakika kwa usalama wa watu na mizigo ni Mv Liemba (Tanganyika), Mv Songea (Nyasa) na MV Serengeti katika ziwa Victoria. Meli ya Mv Victoria imesitisha huduma baada ya kuonekana kutokuwa na usalama.

PESA ZA UKARABATI
Licha ya serikali iliyopita kuahidi meli hizo zingepatikana kabla ya uchaguzi mkuu, hali ya kifedha ilikuwa taabani kwani ilishindwa hata kuchangia fedha za usanifu wa meli mbili mpya katika maziwa ya Tanganyika na Victoria.

Taarifa hizo zinaeleza fedha zilizofanya kazi hiyo zilitolewa na Danida kwa makubaliano kuwa serikali itazirejesha.

Chanzo hicho kilisema baada ya kufanya usanifu huo, Danida ulitangaza zabuni ya kupata kampuni ya kutengeneza meli hizo, mchakato huo unaendelea japo kwa mwendo wa taratibu.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments :

Post a Comment