Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, George Simbachawene amesema hataki kuona mwanafunzi yeyote akikaa sakafuni ndani ya miezi sita ijayo.
Simbachawane aliyasema hayo jana Ikulu jijini, wakati akizungumza na Nipashe, baada ya kuapishwa yeye na mawaziri wenzake.
“Haiwezekani nchi yetu iliyojaa misitu mingi halafu wanafunzi wanaendelea kukaa chini…sitavumilia na nawahakikishia watoto wetu hawatakaa chini tena,” alisema Simbachawene.
Aliwataka wakurugenzi wa manispaa, wakuu wa mikoa pamoja na wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanasimamia majukumu yao kwenda kujua kero za wananchi badala ya kushinda maofisini.
Naye Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba, alisema wataweka mipaka ya matumizi bora ya ardhi ili yajulikane maeneo ya wakulima na wafugaji katika kumaliza migogoro iliyokuwa inajitokeza.
Pia Mwigulu aliahidi kulivalia njuga tatizo la uvuvi haramu ambalo limekuwa sugu katika maeneo mbalimbali nchini.
Nchemba alisema tayari Rais Magufuli alishatoa dira ya mwelekeo kwa kile anachokitaka kifanyike katika wizara hiyo hivyo anajua pakuanzia na itakuwa kazi rahisi kwake.
“Kazi yangu ni kutembea katika maneno ya Rais katika kuhakikisha Watanzania wanapatiwa yale yaliyokusudiwa katika kipindi hiki cha miaka mitano,” alisema Nchemba.
Angela Kairuki ambaye ni Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi na Utawala Bora alisema kiapo chake ni deni kubwa na atahakikisha anatekeleza yale anayotakiwa kuyafanya katika wizara yake.
Alisema atatekeleza majukumu yake kwa kasi ya hali ya juu huku akiwataka watumishi walio chini ya ofisi yake kuwajibika kuchapa kazi na kujiepusha na vitendo vya ubadhirifu wa mali za umma.
Naye Waziri wa Habari, Wasanii, Utamaduni na Michezo Nape Nnauye, alisema atayafanyia kazi mambo mbalimbali yaliyokuwa yanalalamikiwa na vyombo vya habari ikiwamo Sheria ya Habari.
Alisema atafanya kazi zake kwa mujibu wa sheria na taratibu hivyo wananchi wasihofu kwamba ataingiza masuala ya chama.
Naye Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Profesa Posi Abdallah alisema atakwenda kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili walemavu.
Profesa Abdallah alisema changamoto ya walemavu inafahamika hasa masuala ya uhakika wa matibabu hivyo itakuwa kazi rahisi kwake kuwatumikia.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
No comments :
Post a Comment