Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, April 16, 2016

Wagonjwa wa saratani Uganda kutibiwa Kenya

Waziri wa Afya nchini Uganda, Dk Chris Baryomunsi
Kampala, Uganda. Uganda imetangaza kuwa wagonjwa 400 wanaohitaji matibabu ya saratani watapelekwa Kenya baada ya mashine ya kuwahudumia nchini humo kuharibika.
Wagonjwa hao ni kati ya jumla ya wagonjwa 17,000 wanaohitaji huduma ya mionzi.
Waziri wa Afya nchini humo, Dk Chris Baryomunsi aliambia Bunge la nchi hiyo kuwa Hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi imejitolea kusaidia wagonjwa 400 kutoka Uganda.
Gazeti la Daily Monitor, lilinukuu maofisa wa Serikali, inaonyesha kuwa, Uganda kuna wagonjwa 32,000 wa kansa. Asilimia 55 (sawa na wagonjwa 17,600) wanahitaji huduma ya mionzi.
Dk Baryomunsi alisema, Serikali itagharimia usafiri na malazi, huku Hospitali ya Aga Khan nayo ikigharimia matibabu.
Mashine pekee nchini humo ilikuwa katika hospitali kuu ya Mulago ambayo ndiyo taasisi kubwa zaidi ya matibabu nchini Uganda na hushughulikia magonjwa makubwa.
Mashine ya mionzi iliyokuwa Mulago, aina ya Cobalt 60 Ilinunuliwa mwaka wa 1995 na imekua ikiharibika mara kwa mara, licha ya kukarabatiwa.
Baadhi ya wananchi wa Uganda hivi karibuni waliandamana mitaani wakiishutumu Serikali kwa kushindwa kuboresha sekta ya afya.

1 comment :

  1. Инстраграмм являться самой популярной площадкой для продвижения своего бизнеса. Но, как показывает практика, люди гораздо чаще подписываются на профили в которых уже достаточное количество подписчиков. В случае если заниматься продвижение своими силами, потратить на это вы можете очень много времени, поэтому гораздо лучше обратиться к спецам из Krutiminst.ru подробнее https://shanehbum55432.jts-blog.com/16074355/how-to-get-instagram-followers-rapidly

    ReplyDelete