Uhaba wa mafuta ya petroli visiwani Zanzibar, umesababisha shughuli za uvuvi ambazo zinafanywa na wavuvi wanaotumia vyombo vya moto zikiwamo boti kuzorota.
Akizungumza na Nipashe mratibu wa jumuiya ya wavuvi wa Kojani, Omar Mohammed Ali, alisema kuwa hivi sasa Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati Zanzibar (ZURA), imepiga marufuku uuzwaji wa mafuta kwa kutumia vidumu mpaka mtu apate kibali maalum kutoka mamlaka hiyo.
Alisema kutokana na boti wanazofanyia kazi ya uvuvi haziwezi kufika hadi katika vituo vya kuuzia mafuta hulazimika kubeba vidumu kwa ajili ya kuwekewa mafuta.
Aliishauri mamlaka hiyo kuwa na wafanyakazi wao katika vituo vya kuuzia mafuta kuliko kufuatwa ofisini kwao kwa ajili ya kupatiwa kibali hicho.
Alisema licha ya kwamba hawawezi kuuziwa mafuta katika vidumu hadi wawe na kibali kutoka mamlaka hiyo, lakini kiwango cha mafuta wanachouziwa ni kidogo kulingana na mahitaji yao.
“ZURA wameweka utaratibu kuwa wavuvi wauziwe mafuta yasizidi lita 30, tena kwa vituo maalum vya kuuzia mafuta...hizi ni lita kidogo sana wakati baadhi ya boti za uvuvi zinatumia hadi lita 300, '' alisema mratibu huyo.
Alisema kuwa hivi sasa wavuvi wengi wanashindwa kufanya shughuli zao kutokana na kukosa mafuta hayo.
Aidha, alieleza kuwa hivi sasa samaki wameadimika baharini kutokana na hali ya hewa ambayo ni kipindi cha upepo.
Alisema kuwa bei ya samaki hivi sasa imepanda maradufu kutokana na mahitaji makubwa ya samaki kutoka kwa wananchi na uhaba wa samaki baharini.
“Samaki ambaye alikuwa akiiuzwa Sh. 1000 kipindi cha nyuma hivi sasa anauzwa Sh.2000 hii ni kutokana na upepo ambao umesababisha samaki kuadimika baharini na sio sababu ya uhaba wa petroli,” alisema.
Alisema samaki ambaye anapatikana kwa wingi hivi sasa ni aina ya Morali, lakini Changu, Tasi na wengine wamepotea.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati, Khudhaima Bakari Kheri, alisema wamekuwa wakitoa vibali bure kwa wavuvi kwa ajili ya kuuziwa mafuta.
Aliwataka wavuvi kuvumilia katika kipindi hiki ambacho kumekuwa na uhaba wa mafuta ya petroli, hivyo wamedhibiti uuzwaji wa mafuta kwa kutumia madumu.

No comments :
Post a Comment