dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, September 26, 2022

BAADHI YA WATz WA NJE WAISHUKURU SERIKALI KWA HADHI MAALUMU!


*BARUA YA WAZI KWA SERIKALI *
"Kwanza tunaishukuru serikali kwa kusikia kilio cha muda mrefu cha wanadiaspora wa Tanzania na kuamua kukubali kutoa Hadhi Maalumu ambayo itatoa haki za urai wa Tanzania kwa wazawa wa Tanzania waliopoteza uraia wa Tanzania kwa kuchukua uraia nje ya nchi.

Baada ya tamko la rais kuhusu kutolewa kwa Hadhi Maalumu kumetokea kundi la wanadiaspora ambao kwa sababu zao za binafsi ikiwemo upinzani kwa serikali na kutojali maslahi ya watanzania na Tanzania kwa ujumla, wameamua kujikusanya na wanataka wapeleke kesi mahakamani kudai uraia pacha. Hili likiwa ni jaribio la dhahiri la kukwamisha Hadhi Maalumu isitolewe.

Uraia pacha duniani kote si suala la serikali kulazimishwa. Kuna nchi nyingi kutokana na sababu zao hazikubali uraia pacha. Hata hiyo haki ya uraia wa kuzaliwa ni sheria ya nchi. Kuna nchi nyingine mtoto akizaliwa huko hupewa uraia, na kuna nchi nyingine hapewi uraia wa kuzaliwa.

Wazawa wa Tanzania hatukunyimwa haki hii, wote tumepewa uraia wa Tanzania tulipozaliwa Tanzania. Hata hivyo haki hii haimzuii mtu yeyote duniani kunyang'awa uraia wa kuzaliwa iwapo atakiuka sheria za nchi. Hata anaezaliwa Marekani huweza kupoteza uraia wa kuzaliwa iwapo ataukana uraia wa Marekani au kwa kujiunga na jeshi dhidi ya Marekani, kula kiapo cha utii kwa nchi nyingine au akifanya uhaini.

Leo hii duniani, kama ilivyo kwa Tanzania, nchi nyingi sana na nyingine ziko Ulaya ikiwemo Holland, raia wao akichukua uraia wa nje anapoteza uraia wake wa kuzaliwa.

Zaidi ya hayo Hadhi Maalumu ni muafaka kati ya mahitaji yetu sisi wanadiaspora na matakwa ya serikali. Sisi wanadiaspora tutapata haki za uzawa wa Tanzania tulizozipoteza, na serikali itaendelea kuilinda sera yake kukataa uraia pacha.

Uraia pacha una madhara makubwa kwa Tanzania.

1. Tanzania ina wawekezaji wengi wa kigeni ambao tayari wapo nchini zaidi ya miaka kumi. Tanzania ikitoa uraia pacha ni rahisi kwa wawekezaji hao kutimiza vigezo vya kuomba uraia pacha na wakiupata hawatalazimika kulipa kodi za uwekezaji wala kugawana faida na serikali. Hiyo itakuwa ni hasara kwa serikali na taifa kwa ujumla.

2. Nchini Tanzania, tayari matajiri wakubwa wana asili ya nje ya nchi. Na inaminika wanatumia paspoti za nje kwa siri kwa sababu Tanzania hairuhusu uraia pacha. Tanzania ikiruhusu uraia pacha, hakutakuwa na kigezo cha kuwazuia matajiri hawa kutaja uraia wao wa nje na wanaweza kuhamisha mali nje ya nchi bila ya kificho.

3. Tanzania imezungukwa na nchi zenye uhaba wa ardhi aidha kwa udogo wa hizo nchi (Rwanda) au kwa ardhi za hizo nchi kuhodhiwa na matajiri wachache(Kenya). Tumeona mfano hai, wamasai wa Loliondo kufungua kesi Kenya. Ni wazi Tanzania ikiruhusu uraia pacha raia wa nchi kigeni hasa wa mipakani watatafuta namna ya kupata uraia Tanzania. Hata kama ni kwa kusubiri miaka 10 ya kuishi ndani ya Tanzania.

4. Kuna suala la wakimbizi vilevile, Kongo, Rwanda na Burundi, uraia pacha utakuwa na manufaa zaidi kwao kuliko hata sisi wanadiaspora tunaoupigania.

5. Tanzania ina tatizo la ajira, wamachinga na wasio na kazi ni wengi. Mwisho wa siku uraia pacha maana yake ni kualika wagani nchini.

Hiki si kitu cha kuiga Ulaya, Canada na Marekani. Kwa mfano Canada ina ukubwa kama mara kumi ya Tanzania, lakini ina watu watu kama nusu tu ya watanzania. Wanahitaji watu. Marekani kila mwaka inachezesha viza za bahati nasibu kuchukua wageni waingie kwao.

Kuna wanaouliza mbona majirani zetu wametoa uraia pacha? tusisahau Africa ya mashariki Tanzania ni nchi tajiri kuliko zote kwa maliasili hasa ardhi. Bado tuna ardhi zisizopimwa.

Ukiyafikiria yote haya, hii Hadhi Maalumu sio tu ina manufaa kwa serikali na watanzania, ina manufaa hata kwetu sisi wanadiaspora wenyewe kwa sababu inatulinda tusipate ushindani na wageni katika kupata haki za uraia wa Tanzania.

Wanaodai uraia pacha kwa matamanio yao ya kumiliki hati mbili za kusafiria hawafikirii yote haya. Wanasema itakuwa ni uraia pacha kwa wazawa tu wa Tanzania lakini hawasemi haya;

1. Wageni wakitimiza vigezo vya kupata uraia pacha watanyimwaje.

2. Matajiri wa kitanzania wenye asili ya nje wakichukua uraia wa kwao au wa nje na kuhamisha mali bila ya kificho watazuiwaje.

3. Na hizo sheria za kuwapa wazawa uraia pacha na kuwanyima wageni zinatekelezeka vipi ukizingatia Tanzania haina teknolojia kama za Ulaya kwenye kudhibiti data. Na pia ina matatizo ya rushwa na weledi wa utendaji kazi.

Kwa kuzingatia haya yote sisi wanadiaspora ambao tumeridhika na kutolewa kwa Hadhi Maalumu tunaiomba serikali ya Tanzania isituchanganye na hao wanaotaka kufungua kesi mahakamani kudai uraia pacha. Hawawakilishi wanadiaspora wote wa Tanzania. Vilevile tunaiomba serikali iendelee na zoezi la utoaji Hadhi Maalumu ili tuweze kushiriki kikamilifu kuijenga nchi yetu ya uzawa Tanzania".


CAUTION: Any opinion expressed in this blog does not necessarily reflect the view of the blog's owner. 
                   The above article has been quoted from the HADHI MAALUMU DIASPORA TZ platform.

5 comments :

  1. Hizi ni hoja za ovyo sana uliztoa hapa. Zina ubaguzi na zinaakisi ukubwa na upana wa akili ya kila anayeziamini. Jifunzeni kutoka Kenya tu mtuoneshe hayo madhara ya uraia Pacha. Au tuseme Kenya uchumi wale ni mdogo kuliko Tanzania? Acheni kasumba zenu hizo huu ni uongo na wala sisi diaspora ya U.K. hatuwezi kuunga mkono mawazo haya ya kibaguzi na upujufu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani wewe kaka/dada kwenye Hadhi Maalumu utakosa nini? Utapata kila kitu isipokuwa kupiga kura na kuchaguliwa kuwa wazili tu. Au huo uwazili ndio nia yako? Hadhi Maalumu ni sawa sawa na huo Uraia Pacha kasoro kupiga kura tu. Faida tele za Hadhi Maalumu unapewa wewe Mzawa peke yako, lakini faida tele za Uraia Pacha ukipewa wewe atapewa na mtu wa nje. Sasa unataka hizo facilities unazopewa wewe Mzawa apewe na mtu wa nje? Fikiria hapo!

      Unatoa mfano wa Kenya, hivyo Kenya wanajitambua katika kudhibiti raslimali zao? Raslimali zao zote zipo chini ya wageni, au hujui hilo? Hujui pia kwanini wakamkataa Magufuli wa Kenya katika uchaguzi wao wa majuzi? Unataka na sisi Tz rasilimali zetu ziwe chini ya wageni kama Kenya na baadae tuchaguliwe ma-Rais wa kutuongoza?

      Watu hamjafahamu tu, lakini katika hii Hadhi Maalumu you have nothing to lose but everything to gain. Ni wewe Mzawa peke yako ndio utakaefaidika kwenye Hadhi Maalumu na mgeni japokuwa ni raia unamtupa nje. Hadhi Maalumu utapewa wewe Mzawa tu na yule mgeni atapewa uraia kama ilivyo hivi sasa na atafuata sheria zile zile za Mtz. Hadhi Maalumu itakufanya wewe Mzawa uwe juu ya mgeni japokuwa mgeni kapewa uraia, lakini wewe hatokufikia juu ya huo uraia wake aliopewa. Ukipewa Hadhi Maalumu maanake ni kuwa uhusiano wako na Tz upo na wala hautokufa. Sasa sijui tunawasiwasi wa nini. Au tuukubali uraia pacha kwasababu Kenya wameukubali? Tizama hasara zake Kenya kwanza. Mgeni kila siku anazidi nguvu kuliko yule mwananchi. Kwetu hatutaki iwe hivyo!!!!
      Jamani tusirukie tu hizi mila za magharibi. Hazitotusaidia kitu.

      Delete
    2. Usitupotoshe, kwa nini mzawa awe na hadhi maalum, yeye ni mzawa na ana haki hata aende wapi, unachoongea ni kutaka kuwapotosha wasioleelewa tu.

      Delete
  2. Nafikiri unayedai Hadhi Maalumu utakuwa uwezo wa kufiri ni mdogo zaidi au ni Mrundi ila unajificha kwenye hadhi maalumu.
    Maana hoja zako zinaonyesha hauja hudhuria shule kabisa Kwa hiyo hujui Hata unachoandika.
    Kuzaliwa Tanzania ni haki Yako ya msingi hakuna mtu Wala Taasisi yeyote inayoweza kunyang'anya Sasa Wewe unaposema unaishukuru Serikali Kwa kuwuhurumia kukupa hadhi maalumu how? Utakuwa ubongo hauko sawa.
    Kamshukuru mama yako kukuzaa Tanzania siyo Serikali yaani Serikali inafanya ubaguzi wa kukubagua alafu unaishukuru huo ni upuuzi ushamba na wendawazimu. badilika kijana
    Siku nyingine ukiandika Upuuzi Kama huu weka na majina Yako.
    Hata Kama unatumiwa na CCM hapa umezidi.
    By; George Emanuel Mwaipungu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ahsante Ndugu Mwaipungu. Nishamshukuru mama yangu kwa kunizaa Tanzania. Nisamehe, kwani nilikuwa nimelewa Chibuku!

      Delete